Header Ads Widget

Unaikumbuka ile movie ya Transformer? Waturuki watengeneza gari linalofanana na maroboti ya katika transformer

1

Ulimwengu wa muvi umekuwa na mchango mkubwa sana katika kuleta teknolojia mpya ulimwenguni. Tumeona uvumbuzi wa simu za touch ulianzia kwenye muvi na sasa imekuwa kitu cha kawaida sana. Hii haijaishia kwenye simu, mpaka kwenye maroboti yenye uwezo wa kufanya vitu vikubwa zaidi.
Kama wewe ni mpenzi wa muvi utakuwa ushaelewa hapa nini najaribu kuzunguzia. Katika muvi za Transformer magari yanageuka kuwa maroboti yenye uwezo wa kutembea na kufanya mambo mengi.
Kampuni moja ya kituruki inayofahamika kama Letvision imetengeneza moja ya magari yanayofanana kabisa na yale ya katika muvi za Transformer walilolipa jina la Letrons kutoka katika series ya magari ya BMW Series 3.
Lilitengenezwa kwa miezi 8 na timu ya wahandisi 12 na wasaidizi 4 tuu. Angalia video yake hapa kufahamu zaidi.


Post a Comment

0 Comments