Wakati huku kwetu bado wanafunzi wanaendeleza njia za kizamani na kubuni mpya za kuibia majibu au kufanya udanganyifu wakati wa mtihani, wanafunzi wa nchini China ndio wanaongoza katika matumizi ya teknolojia ya kisasa katika kufanya udanganyifu huo.

Kali zaidi imetokea hivi karibuni baada ya kugundulika ya kuwa vijana wameendelea zaidi kiteknolojia katika kuhakikisha wanafanikiwa katika kuibia kwa kutengeneza miwani ambayo inarekodi na kutuma picha hizo kwa mwingine. Hii ni katika mtihani maarufu zaidi ujulikanao kwa jina la Gaokao ambao unaweza kuufananisha na ule wa kuhitimu kidato cha sita kwa hapa bongo. Ukaguzi wa wanafunzi kuingia eneo la kufanya mitihani katika gaokao imebidi nao uwe wa kiteknolojia ya juu, na hivyo imekuwa kama vile mwanafunzi anapita uwanja wa ndege.

Afisa Usalama akionesha Miwani aliyokamatwa nayo mwanafunzi

 

Hivi kijana wa kibongo akipata vifaa hivi si atafaulu mitihani yote hapa bongo, au wewe unaonaje?