Kutokana na kusitisha uzalishaji huo, Jumanne hii uongozi wa kiwanda hicho ulitoa taarifa kwa vyombo vya habari kupitia Ofisa Mtendaji Mkuu Tanzania, Harpreet Duggal kuwa shughuli za uzalishaji kwa wiki moja iliyopita zimeathirika zaidi.
“Gharama kubwa za uzalishaji zilizopo unapolinganisha na gharama za nchi nyingine za uzalishaji katika Dangote, utaona uendeshaji hapa Tanzania upo juu mno, moja ya sababu kuu ni matumizi ya jenereta za dizeli katika kuendesha kiwanda,” alisema.
“Lakini pia kiwanda kuwa mbali na soko kuu la saruji kumechangia ongezeko la gharama za usafirishaji, nategemea serikali inaangalia suala hili la gharama na jinsi ya kutafuta njia ya kutupunguzia mzigo huu,” alisema Duggal.
“Tuna matumani makubwa kuhusu uwekezaji wetu wa muda mrefu hapa Tanzania, tupo makini kwa kushirikiana na serikali , tutaweza kuhimili gharama za uzalishaji ili kuendelea kufanya bidhaa ya saruji kuwa na bei nafuu kama ambavyo tumeanza kufanya,”aliongeza.
Aidha Duggal alisema tatizo hilo ni la muda tu na limetokana na hitilafu za kiufundi katika mitambo ya kiwanda hicho na kwamba mafundi wapo kazini na shughuli za uzalishaji zitarejea siku chache zijazo. Kiwanda hicho kinadaiwa kusimamisha uzalishaji kwa kipindi cha zaidi ya wiki tatu sasa, kutokana na kuelemewa na gharama za uendeshaji.
0 Comments
on