Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda chupuchupu imtumbue mwenyekiti wa Mtaa wa Temboni kata ya Msigani Ubungo, Israel Mushi kwa hutuma za kuhusika katika ujenzi wa barabara hewa kutoka Msuguri mpaka Msingwa na badala yake msaha huo kuhamia kwa watendaji wawili wa zamani wa Kata ya Msigani kwa kuhusika ma mradi huyo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa kata ya Msigani
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda akizungumza na wananchi wa kata ya Msigani
Wakizungumza kwa hasira mbele ya mkuu wa mkoa, Wananchi hao amelalamikia kuchangishwa pesa mara kadhaa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo huku wakidai walifanya hivyo baada ya kuambiwa barabara hiyo haikuwa katika mgango wa Halmashauri wala Tanroad.
“Barabara hii imekuwa ikitusumbua kwa muda Mh mkuu wa mkoa na tumekuwa tukichangishwa pesa kwa ajili ya ukarabati wa mara kwa mara lakini tunasikia hii barabara ilitengewa milioni 17 na Halmashauri kwa ajili ya ukarabati mwaka uliopita lakini hatujui hizo pesa zielenda wapi kwa sababu barabara haijawai kutengenezwa,” aliongea mmoja kati ya wananachi wa eneo hilo aliyejitambulisha kwa jina la Moreen Gombe.
Hatua hiyo ilimfanya mkuu wa mkoa, Paul Makonda kumtaka mwenyekiti wa mtaa huo, Israel Mushi kueleza kiundani juu ya mradi huyo.
“Mh Mkuu wa Mkoa hii barabara ni kweli kuna watu wanachangishana pesa kwa sababu hii barabara tumeambia haipo katika mpango wa Halmashauri. Mimi baada ya kufikishiwa hilo nikawaambia siwezi kujihusisha kwenye mradi huyo, kama mmeamua kufanya hivyo fanyeni lakini mimi sipo na suala la pesa milioni 17 za Halmashauri mimi silijui anayeweza kulizungumzia hilo ni mtendaji wa kata ambaye aliidhinisha huo mradi,” alisema mwenyekiti huyo.
Mwenyekiti wa mtaa wa Temboni, Israel Mushi
Mwenyekiti wa mtaa wa Temboni, Israel Mushi
Baada ya Makonda kupata ufafanuzi huo, alimtaka mtendaji wa kata ya Msigani, Eutropia Kimati kufafanua matumizi ya milioni 17 walizopokea kutoka kwa Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa barabara.
Mtendaji kaya ya Msigani, Eutropia Kimati akieza jambo
“Mh kwanza mimi ningependa kusema kwamba nina miezi mitatu toka niteuliwe kuwa mtendaji wa kata. Lakini file la mradi huo nililikuta ofisini kwangu, kwa hiyo waliohusika kwenye mradi huo ni mtendaji kata aliyepita Neema Kalumba lakini aliyeupitisha huu mradi alikuwa ni Zuhura Almas ambaye alikuwa hapa kabla ya Neema,” alisema Kimati.
Kauli hiyo ya mtendaji kata ilimfanya mkuu wa mkoa kumwagiza RPC wa Kinondoni, Suzan Kaganda kumkatama mtendaji huyo kwa ajili ya kujibu tuhuma hizo.
Pia Makonda ameitaka TAKUKURU kuchunguza tuhuma za ufisadi huo ili kuwatia hatiani wote waliohusika katika ufisadi wa mradi huo
0 Comments
on