Header Ads Widget

Mahabusi waliojaribu kutoroka watiwa mbaroni

Mahabusi wawili kati ya saba waliotoroka chini ya
ulinzi wa askari wa Jeshi la Polisi katika eneo la
Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Kilimanjaro,
wametiwa mbaroni na kuhukumiwa kutumikia
vifungo jela.
Kutoroka kwa mahabusi hao kulisababisha askari
10 mkoani Kilimanjaro waliokuwa wakiwalinda
kushikiliwa na polisi kwa mahojiano.
Mahabusi hao ni Lucas Akaro (26) ambaye
alijisalimisha kwa uongozi wa Gereza la Karanga
na Charles Malenge (24), aliyekamatwa na Polisi
akiwa amejificha nyumbani kwake.
Wakati wakitoroka, Akaro alikuwa akikabiliwa na
kesi ya mauaji ya mwanafunzi wa mwaka wa tatu
chuo cha udaktari KCMC, Baneti Materu (22) na
Malenge ya unyang’anyi.
Mahabusi hao walifikishwa kortini jana mbele ya
Hakimu Mkazi Mfawidhi, Joachim Tiganga na
kukiri shtaka moja kati ya mawili yaliyokuwa
yakiwakabili.

Post a Comment

0 Comments