Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli, leo tarehe 04 Novemba, 2016 atafanya mahojiano ya kwanza na waandishi wa habari tangu aingie madarakani mwaka mmoja uliopita.
Mahojiano
haya yatarushwa moja kwa moja na vituo vya habari vya redio na
televisheni kutoka ukumbi wa Ikulu Jijini Dar es Salaam na yataanza saa
4:00 asubuhi.
Kurugenzi
ya Mawasiliano ya Rais inapenda kuwaalika wananchi wote kusikiliza na
kutazama mahojiano hayo ili mpate fursa ya kujua mambo mbalimbali ambayo
Mheshimiwa Rais atayatolea majibu.
Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
0 Comments
on