ILIPOISHIA
"KAMA MIMI SIJAKUWEKA, TUMBONI MWAÑGU MIEZI TISA, HUTO MUOA SHEILA, ILA KAMA NILIKUZA KWA UCHUNGU, BASI UTAMUOÀ SHEILA."
"HICHO
KIBESI CHAKO WAPANDISHIE HAO WASICHANA WAKO, ILA SI MIMI MAMA YAKO.
USIPO ANGALIA NITAMPOTEZA HUYO MBWA WAKO NA KITOTO CHAKE"
Mama
alizungumza na kupiga hatua tatu mbele akanigeukia na kwaishara ya
kidole chake, akaniamrisha nitangulie kwenye gari, huku yeye na mlinzi
wake wakifwatia nyuma.
ENDELEA
Katika siku ambayo nimejisikia vibaya ndani ya moyo wangu ni siku ya
leo, sikutegemea kama mama yangu anaweza kumkataa mwanangu mbele yangu
japo sijamuona, ila muonekano wa kwenye picha una dhihirisha kwamba
Junio ni mwanangu wa damu. Kila nilipo mtazama aliye keti, pembeni ya
siti yangu. Moyo ukazidi kuniuma, kiasi cha kutamani nishuke ndani ya
gari, nitembee hata kwa miguu kurudi nyumbani.
Tukaafika
nyumbani nikawa wa kwanza kushuka ndani ya gari. Sikuelea chumbani
kwangu kuepusha kelele za Sheila, ambaye muda wote, mama anamchukulia
Sheila kama mtoto mdogo. Chochote anacho kihitaji anakipata.
"Shem, mbona umekaa huku bustanini, peke yako”
Sauti ya ndugu wa Sheila anaye itwa Blanka, niliisikia ikinisemesha, nyuma yangu
"Hapana nina punga punga upepo"
"Ahaaa, basi nilijua kwamba hjarudi na mama"
"Nimerudi"
Blanka akakaa pembeni yangu, huku akivua viatu vyake na kuvisogeza pembeni
"Shem mbona kama, haupo sawa, unaumwa?"
Nikatingisha kichwa kumjibu Blanka
"Sasa n nini tatizo shem wangu? Sasa hivi ulitakiwa uwe ndani unafuraha"
"Hapana, nina furaha"
"Shem huna furaha, au dada amekudhi?"
"Hapana, kuna maswala yangu yakibiashara kidogo ndio ninayafikiria"
"Ahaaaa, ila shem kuna kitu nahitaji kukuuliza"
"Kitu gani?"
"Unampenda kweli dada Sheila?"
Ikabidi nimtazame Blank vizuri machoni mwake.
"Mbona umeniuliza hivyo?"
"Yaa nà hitaji kujua, kwa maana kuna vitu hapa nyuma vilikua vinaendelea"
"Sijakuelewa, vitu gani vilikua vinaendelea?"
"Kuna
mambo alikua anayafanya dada Sheila, kwa upande wangu sijayapenda
isitoshe anakwenda kufunga ndoa na wewe, sizani kama anastahili kua
mkeo"
Moyo ukaanza kunienda mbio, nikamgeukia vizuri Blanka, kabla sijamuuliza kitu, nikamuona mama akija sehemu tulipo.
"Ina bidi uongeze juhudi kwenye masomo, isitoshe unasoma masomo ya udaktari, ujitahidi sana"
Ilinibidi
kubadilisha mada, ili mama asielewe ni kitu gani tunazungumza.
Chakumshukuru Mungu Blanka alinielewa maana yangu ya kubadili mada
tuliyo kua tukiizungumza.
"B wezako wanakutafuta kule ndani"
"Ahaa sawa mama"
Blanka akanyanyuka na kuondoka, mama akakaa sehemu nilipo. Ukimya wa sekunde kadhaa ukakatiza, sikua na kitu cha kuzungumza.
"Hivi Eddy, ni nani aliye kuroga?"
"Hakuna"
"Nimempigia mchungaji simu, aje kukuombea"
"Ili iweje"
"Eddy wewe si bure, utakua umerogwa"
"Mama na elimu yako hiyo yote yaani una amini kwamba mimi nimerogwa?"
"Tena sana, na aliye kuroga amesha fariki"
Laiti
kama añgekua si mama yangu, aliye nibeba tumboni mwake miezi tisa,
ningemtandika ngumi, ambayo asinge isahau maisha yake yote.
"Na
kama nilivyo kuambia, mtoto uliye naye mimi simtambui, na huyo mama
yake naye simtambui. Sasa ole wako unidhalilishe kwa wageni nilio
waalika. Haki ya Mungu naapa nitakuachia laana."
Mamà akanyanyuka, nakujifunga tenge lake vizuri.
"Na sitaki siku hata moja huyo mwanangu Sheila ajue, kwamba unamtoto. Akijua na kuchukua maamuzi mabaya utajuta"
Mama à kaondoka na kuniacha nikibaki nikimsindikiza kwa macho, yaliyo jaa hasira.
Kitu
kilicho anza kuniumiza kichwa, nikuhitaji kujua ni mambo gani aliyo kua
akiyafanya Sheila, kipindi ambacho mimi sikuwwepo. Nikaanza kuamini
kwamba Blanka atakua ni msaada mkubwa sana kwangu.
Usiku
sikuamini kumuona mchungaji akiwa ameketi kwenye sofa za sebleni,
akizungumza na mama. Wakaniita, nikajumuika nao kwenye mazungumzo, mimi
na mchungaji tukaingia kwenye chumba cha maombi, kilichopo ndani ya hili
jumba jipya la mama.
Bila hata mchungaji kuniuliza swali, lolote akaanza kuniombea huku akiuweka mkono wake juu ya kichwa changu
"Pepo mchafu uliyopo ndani ya kichwa cha huyu kijana toka kwà jina la Yesu kristo"
Mchungaji aliendelea kuniombea huku akinisukuma sukuma kichwa changu. Zaidi ya nusu saa mchungaji aliendelea kunisalia
”Mchungaji, nimechoka kupiga magoti kama mapepo sina si tuachane na hii biashara bwana"
"Ohhhh shagara bagharaa, pepo wewe mchafu huwezi jibizana na mimi mtu wa Mungu, hapo ulipo toka kwa jina la Yesu"
"Mchungaji tuheshimiane bwana, sina pepo wala nini. Hembu fanya jengine la maana"
"Pepo pepo mchafu tokaaaaaa"
Nikaona mchungaji hanielewi, nikasimama, akabaki kunitazama machoni mwangu, huku akizungumza maneno, nisiyo yaelewa.
”Nisikilize
mchungaji, nahisi huyo Mungu iyepo ndani yako sidhani kama ni Mungu
huyu tunaye muabudu. Hembu rudi ulipo toka kasime vizuri hiyo biblia
yako uje tena kuniombea. Matatizo yaliyopo hapa ni kati yangu mimi na
mama yangu sawa?"
Nilizungumza
kwa sauti ya ukali na yachini, jambo lililo mfanya mchungaji
kunitumbulia mimacho. Nikafungua mlango na kwenda chumbani kwangu, na
kulala.
Asubuhi na mapema, nikaamka. Nikafanya mazoezi kama kawaida yangu,
nikaenda kwenye nyumba wanayo ishi watoto wa kike, na ndipo anapo kaa
Sheila, nilitenganishwa nà ye ili nisimuone hadi siku ya harusi yetu.
Nikamtafuta Blanka ila sikumuona
"B amekweñda wapi?"
"Wametoka na bibi harusi, leo wamekwenda saloon kuanza kupambwa"
"Saloon gani?"
"Labda mpigie wifi mwenyewe umuulize"
Nikaachana
na mdogo wangu, ambaye nilitambulishwa sikujua hata ametokea wapi, ila
wote ni ndugu. Nikampigia simu Sheila ila haikupatikana, nikajaribu
kupiga simu ya Blanka ñayo haikupatikana. Nikajaribu kupiga ya ndugu
mwengine niliye hisi atakua mpambe kwenye msafara huo, simu yake ikaita
baada ya muda akaipokea
"Dada upo na hao maarusi?"
"Ndio, tupo Saloon moja inaitwa Rich Power Women au R.P
W"
"Ipo wapi?"
"MÃ eneo ya huku posta"
Akanielekeza walipo, akanieleza simu za Sheila na Blanka, zimezima chaji.
Nikaingia
kweñye moja ya gari, kwa lengo la kwenda kuzungumza na Blanka, nikafika
getini nikashangaa kuona halifunguliwi na askari wanao linda.
"Vipi fungueni basi geti"
"Muheshimiwa ametuambia kwamba wewe hà uruhusiwi kutoka"
"Nini?"
"Ndio, tunafwata agizo lake, samahani kwa usumbufu muheshimiwa"
Askari mmoja, aliniambia huku akiwa ameshika bunduki yake aina ya SMG pamoja na mbwa mkubwa, na anaye onekana mkali sana.
Nikatoa simu yangu na kumpigia mama, aliye kwenda kazini, alfajiri na mapema.
"Mama ni mambo gani unayo nifanyia lakini?"
"Mambi gani?"
"Ndio umewapa amri hawa askari wako mimi nisitoke nje?"
"Ndio, utatoka kesho siku ya harusi yako tu. Hiyo sio ombi bali ni amri"
Mama
akakata simu, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, huku nikihema kwa
hasira. Ikaingia namba ngeni kwenye simu yangu, iliyo nistua sana moyo
wangu. Taratibu nikaipokea na kuiweka sikioni mwangu.
"Haloo bwana Eddy"
Nilisikia sauti ya kiume
"Nani wewe?"
"Hauna haja ya kujua mimi ni nani, Ila nina habari njemaa sana kwako"
"Una masaa ishirini na nne, kuleta kiasi cha pesa milioni mia moja, kumuokoa mke wako na mwanao Junio, la sivyo WATAKUFA"
"Wewe ni na.....?"
Simu ikakatwa, nikabaki nikiwa nimeitazama simu yangu, mapigo ya moyo yakinienda mbio.
SORRY MADAM 84
Nikageuza
gari langu, nikalirudisha sehemu nilipo lichuku.Nikashuka haraka na
kuelekea chumbani kwangu. Kitu cha kwanza kukifanya, nikachukua kadi
zangu mbili za benki, nakuziweka kwenye mfuko wa jinzi niliyo ivaa.
Nikachukua sweta langu lenye kofia, japo Dar es Salaam kuna joto kali,
ila ikanilazimu kulivaa, hivyi hivyo. Nikasimama nje ya chumba changu
kilichopo ghorofani, kila mtu nikamuona anashuhulika na mambo yake.
Kitu
kinacho zidi kuniumiza kichwa ni jinsi ukuta wa jumba hili ulivyo
mrefu, huku juu ukiwa umezungushiwa nyanya zilizo na umeme wenye volt
nyingi sana.
"Chaji"
Nilijisemea
mwenyewe, nikachukua chaji ya simu yangu. Nikatoa walet yangu mfukoni,
nikaikuta ina noti mbili za dola mia pamoja na na shilingi elfu sabini.
Chakushukuru Mungu, nikaliona gari lakukusanya mataka taka likiingia
getini, nikashuka kwa haraka pasipo kusemeshana na mtu, nikafika sehemu
lilipo simamishwa, ambapo wafanyakazi wake wapo bize kwa kukusanya
matakataka yaliyopo kwenye mindoo mikubwa.
Kwa
haraka nikabingiria kwa haraka na kuingia chini, ya gari hili kubwa la
taka taka. Nikashikilia kwenye, bomba zilizopo chini ya gari hili. Baada
ya dakika kumi, wakawa wamemaliza, tukafanikiwa kutoka getini pasipo
askari kugundua kitu cha aina yoyote. Kutokana gari hili linapita kwa
kila nyumba zilizopo kwenye maeneo ya nyumba za eneo hili, likasimama
kwenye nyumba ya tatu kutoka lilipo jumba la mama.
Nikatoka
chini ya gari pasipo mtu kuniona. Nikakodi pikipikia kuelekea benki ya
posta. Niliwa njiani simu yangu ikaita, ikawa ni namba ngeni, ila ni
yatanzania.
"Mmm"
"Shem mimi Blanka upo wapi?"
"Naelekea benki ya posta, upo wapi?"
"Nimetoka
huku saloon nimeazima simu ili nikupigie, sijui tunaweza kuonana sasa
hivi, kwa maama leo hatuto rudi nyumbani na kesho ndio harusi yako"
"Upo wapi?"
Manka
akanielekeza sehemu alipo, ikanilazimu kughairi safari ya benki na
kwenda alipo yeye. Ilituchukua kama dakika kumi na tano kufika alipo
Blanka kwenye mgahawa mmoja ulio jificha sana, kutona na uwenyeji wa
dereva huyu wa bodaboda, aliweza kupafahamu. Nikamlipa dereva pesa anayo
nidai, nikaingia ndanibya mgahawa kama Blanka alivyo nielekeza,
nikamuaona amekaa kwenye kona moja ya huu mgahawa ambao si rahisi mtu
yoyote kumuona, kutokana na kigiza kilichopo ndani ya huu mgahawa.
"Mbona shemu umevaa hivyo?"
"Mama alikua haitaji mimi kutoka nje'
"Ahaaa sasa hapa napata picha"
"Picha gani?"
"Nilimsikia akizungumza asubuhi na dada Sheila, kwamba huto toka, sasa sikuwaelewa wanamaanisha nini"
"Ehee kabla hujaniambia ulicho hitaji kuzungumza jana, mbona umetumia namba ambayo si yako?"
"Nimehofia
kutumia namba yangu kuwasiliana na wewe kutokana toka juzi namba za
watu wote mule ndani zimeunganishwa na namba ya mama, zikiingia na
kutoka lazima kwake zipitie"
"Mmmmm hata yangu?"
"Yako sijajua, ila nahisi pia itakua kwenye mlolongo huo huo"
"Poa tuachane na hilo, wewe na Sheila muma undugu wa kivipi?"
"Ahaaa ni story ndefu kaka yangu, ila kiufupi Sheila si ndugu yangu wa kuzaliwa wala wa ukoo"
"Sheila
nilimsaidia kipindi fulani alitekwa, sasa nilimuokota porini akakaa
sana kijijini kwetu Tulimuuguza hadi akapata nafuu ndipi alipo rudi
huku, akaamua kulipa fadhila zake kwa kuniendeleza na masomo"
"Ahaaaa kwa maana nilikua ninajua Sheila hana ndugu"
"Kweli hana, mimi ni ndugu yake wa hiyari"
"Kitu
nilicho hitaji kukuambi wewe kama kama yangu, Sheila anatabia zilizo
nipelekea leo kuzungumza hichi nimacho taka kukizungumza"
Blanka akashusha pumzi na kunitazama usoni, kisha akapiga fumba la juisi yake aliyo agizia.
"Kabla hawajaja kuja huku marekani, dada sheila alikua akinilazimisha kumtoa mimba aliyo kua nayo"
"Ng....ngooja kwanza, kimba gani?"
"Hii aliyo kua nayo, kwani kipindi anakuja huko ulipo kua, alijigundua ana mimba ya ya wiki kam moja na nusu"
"Ñgoja mimba ya wiki inaweza kuonekana?"
"Ndio inategemea na maumbile ya mwanamke wengine hadi mwezi ndio wanaiona"
"Basi nilikataa kumtoa, akaniambia atajua nini cha kufanya. Alipo kuja huko sijui kama mulikutana kimwili au laa?"
Kwa upande mmoja kichwa kikaanza kunikoroga kwa hasira, huku upande wa pili ikiwa ni nafuu kwangu kuepukana na jukumu la ndoa.
"Nilikutana naye"
"Na umaamini mimba ni yako?"
"Mi sijui?"
"Kwani siku ulipo onanana naye alikuaje?"
"Mimi wala sielewi hapa nahisi kuchanganyikiwa"
"Tulia shem wangu, ila kuna kidhibitusho kingine ñgoja nikuonyeshe"
Blanka
akatoa simu yake, akaminya minya na kunipa niangalie baadhi ya meseji
alizo zipiga picha zikiwa kwenye simu ya Sheila zikionyesha akijibizaba
na mwanaume aliye mtia mimba.
Sheila alikakua à kimlazimisha mwanaume huyo, akubali yeye kutoa mimba kwani mumewe amesha rudi.
"Huyo jamaa yake unamjua?"
"Ndio, tena ngoja nikuonyeshe"
Blanka akachukua simu yake akaminya minya baadhi ya sehemu anazo zijua mwenyewe, akanikabidhi tena simu yake.
Moyo wangu ukazidi kukosa amani, baada ya kumuona John akiwa amekbatiana na Sheila, tena wakinyonyana midomo yao
"Huyo jamaa, anadai anafanya kazi kwenye shirika la ndege la Ufilipino, na huja mara chache sana hapa Tanzania"
Mwili
mzima ukazidi kunitetemeka kwa hasira kali, huku nikimtazama John
ambaye hadi sasa hivi, amechukua kila kitu kutoka kwenye mikono yangu.
Kuanzia mali za baba yangu hadi Sheila mwanamke niliye tokea kumuamini
sana.
"Alafu
hafi sasa hivi, kuna mpango ambao Sheila ameupanga na huyo jamaa yake,
sasa sijajua ni mpango gani. Mara nyingi Sheila ananiambia mambo
yanakaribia kuiva, tutakua matajiri sana"
”Ila shem ninakuomba usinitaje, kwani Sheila anaweza kuniua mimi"
"Hawezi kukuua, nakuomba ufwatilie huo mpango ulio jificha"
"Sawa nakuahidi nitalifanya hilo, na vipi huto jamaa unamjua?"
"Hapana?"
"Mbona anajuana sana mama, na huwa anakuja nyumbani, anadai ni rafiki yako?"
Kabla sijamjibu Blanka simu yangu ikaingia meseji kwa namba iliyo nipigia mara ya kwanza kutoka Somalia
(Jinsi unavyo kaa kimya, ndivyo jinsi unavyo karibisha vifo vya familia yako)
"Shitiii"
Nikajikuta
nikiibamiza simu mezani, kabla haija anguka chini, Blanka akaiwahi
kuidaka, akausoma ujumbe ulio ingia kwenye simu yangu
"Ni familia gani?"
"Nitakuambia, fanya urudi Saloon, ila usimuambie mtu yoyote chochote kuhusiana na kuonana kwetu"
"Sawa nimekuelewa shem"
"Ukiinipigia simu piga kwa namba nyingine kama vipi tafuna namba mpya"
"Sawa niyafanya hivyo shem"
Nikawa wa kwanza kutoka ndani ya mgahawa, nikakodi pikipiki hadi benki ya posta, nilipo hifadhi kiasi changu kikubwa cha pesa.
"Samahani, nahitaji kutoa pesa"
"Nilizungumza na jamaa, mmoja ambaye ni muhudumu"
"Chukua fomu ya kutolea hapo juu"
"Sihitaji fomo hiyo kwani nataka kutoa kiasi kikubwa cha pesa"
Muhudumu akanitazama kwa macho ya mshangao
"Unataka kutoa kiasi gani?"
"Milioni mia na hamsini"
"Mmmmm, ngoja nikukutanishe na meneja, nisubirie hapo"
Jamaa
alaondoka na baada ya kuda akarudi na kuniomba niongozane naye,
nikaingia ofisini kwa meneja, nikamueleza shida yangu niliyo nayo,
akaniomba namba ya accounti yangu, nikampa akaminyaminya batani za
computer yake, kisha akanitazama huku alivua miwani yake.
"Samahani, bwana Eddy hii akaunti yako imefungiwa"
"Imegungiwa?"
"Ndio na agizo hilo, hili limetoka ofisi ya waziri mkuu, masaa kama mawili yaliyo pita"
"Sababu?"
"Ahaaa tumeambiwa tuifunge kwa à gizo la waziri mkuu"
"Asante"
Nikachukua
kadi yangu, na kutondoka sikutaka kuuliza nini chanzo cha akaunti yangu
kufunguliwa kwani natambua mama ndio chanzo. Nikaenda benki ya bacrays
ambapo, nikakutana naajibu ya kufungiwa, kwa akaunti yangu mbaya zaidi
sina akaunti nyingine zaidi ya hizi mbili.
Nikaipiga namba ya simu ya Phidaya, ikaita kwa muda na kupokelewà na jamaa aliye nipigia simu muda asubuhi
"Nimazo pesa zenu, niambieni ni wapi mupo nizilete"
"Ohoo Mr Eddy, fwatà maelekezo tutakayo kupa"
"Kwanza kabla sijaonana na nyinyi, nahitaji kuzungumza na mke wangu"
"Subiri"
Baada ya dakika moja, simu akakabidhiwa Phidaya
"Eddy usitoe chochote"
Sauti
ya Phidaya ilisikika, ikiambatana na mlio wa risasi kisha simu
ikakatwa, nikajaribu kupiga tena huku mwili mzima ukinitetemeka ila
haikupatikana tena, na saa yangu ya mkononi ikinionyesha yamesalia masaa
kumi na tano tu.
Usikose kufuatilia sehemu inayofuata kupitia djadam64.com
0 Comments
on