Header Ads Widget

Tunataka turudishe nidhamu ya pesa katika jamii – Nape

Serikali imesema kupungua kwa mzunguko wa fedha hivi sasa kunatokana na dhamira ya serikali ya kujenga mazingira bora ya uchumi ambayo pia yatarudisha nidhamu na matumizi ya fedha katika jamii.

Kauli hiyo imetolewa Waziri wa Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo, Nape Nnauye, wakati akizungumza katika mkutano wa kuanisha fursa za biashara uliondaliwa na ubalozi wa India ukishirikiana na TCIAA mkoani Tanga. Waziri huyo alisema akisema kipindi hiki kumekuwa na tasfiri nyingi kuhusu uchumi na hali ya uchumi nchini.
“Serikali kuu tunatambua kwamba yapo maneno kwamba pesa mtaani haipatikani kweli si kweli?” alihoji. “Kuna watu wanasema hali ngumu sana mtaani tumekuwa hatujui limekuwa tatizo, lakini kwasababu hii tunajua na haijatokea bahati mbaya. Tunataka turudishe nidhamu ya pesa na matumizi ya pesa katika jamii yetu ili kazi halali ziheshimike.”
“Tulianza kufikia mahali kila mtu alikuwa anatamani afanye kazi za dili na hizo ndizo zilizokuwa zinaongeza mzunguko wa pesa ambao huzitolei jasho,” alisema Waziri Nape

Post a Comment

0 Comments