Chama
cha ACT-Wazalendo kimemkumbusha Rais John Magufuli kutekeleza ahadi
yake aliyoitoa katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu wa mwaka
jana, kuwa serikali yake haitaruhusu mwanafunzi atakayefaulu kwenda chuo
kikuu ambaye atashindwa kujiunga na elimu hiyo kwa kukosa ada ama
mkopo.
Katibu
wa Itikadi, Mawasiliano na Uenezi wa ACT, Ado Shaibu leo amesema chama
hicho kimetoa tamko hilo, baada ya takwimu zilizotolewa hivi karibuni na
Bodi ya Mikopo kwa Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HELSB) kuthibitisha kuwa
takribani wanafunzi 65,000 wenye sifa za kujiunga na elimu ya juu,
wanafunzi 20,000 ndiyo waliopata mikopo.
“Kwenye
mikutano yake ya kampeni Rais Magufuli alitamba kuwa serikali yake
hakuna mwanafunzi ambaye atafaulu kwenda chuo kikuu ambaye atashindwa
kujiunga na elimu hiyo kwa kukosa mkopo. tunamtaka kutekeleza ahadi yake
kwa vitendo.”
Ameongeza
kuwa “Kwenye mikoa mingi iliyotembelewa viongozi wa chama wamepinga
vikali utaratibu wa sasa wa utoaji mikopo wa elimu ya juu ambao kama
ukiachwa bila kupingwa utafanya watoto wengi kutoka familia masikini
washindwe kujiunga na elimu ya juu kwa kukosa mikopo,”
Shaibu
amedai kuwa, kisingizio kinachotolewa na serikali cha kutilia mkazo
kwenye kozi za kipaumbele hakistahili kutumiwa kwa kuwa ni kigezo cha
kuwanyima watoto wa masikini haki ya kujiunga na elimu ya juu.
“Katika
ilani ya ACT ya mwaka 2015 suluhisho la mikopo ya elimu ya juu
limepambanuliwa vyema. kifungu 5.4.2 (v)(d) ya ilani yetu inapendekeza
kuanzishwa kwa utaratibu wa scholarship kwa kozi za kipaumbele ili mkopo
utumike kusomesha wanafunzi wengi zaidi wa kozi zinazosalia,” amesema.
0 Comments
on