Mgogoro mkubwa wa ardhi kati ya wananchi wa Likuyuseka wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma na Chuo cha mafunzo ya  uhifadhi wa maliasili ambapo wananchi wanadai eneo hilo la ukubwa wa hekta 3000 linalomilikiwa na chuo hicho  ni mali yao huku wakichangishana pesa kwenda kumuona Rais Dkt John Magufuli ili kutatua  mgogoro huo.

Wakizungumza katika mkutano wa hadhara wanasema kuwa maeneo hayo yameporwa na chuo hicho na wao wanakosa ardhi ya kulima na wanapolima wanakamatwa na polisi na askari wa maliasili na kwamba wao walitoa majengo yaliyokuwa kambi ya wakimbizi wa Msumbiji na si ardhi.

Wanasema kuwa kutokana na mgogoro huo wamekuwa wakinyanyaswa wanapojaribu kwenda kulima maeneo hayo hivyo wanachangishana pesa kwenda kumuona Rais Magufuli kwa utatuzi wa mgogoro huo.

Kwa upande wake Katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo Bw.Haridi Nchimbi anakiri kuwepo kwa migogoro ya ardhi katika wilaya ya Namtumbo ukiwemo wa likuyuseka inayotokana na wananchi kutokujua mipaka yao huku akiwataka kufuata sheria.