**
Zuku TV imezindua kwa upya chaneli ya Zuku Swahili ambayo itakuwa na vipindi vipya vya kusisimua vilivyoandaliwa kwa ajili ya wateja wa Tanzania.
Zuku Swahili inalenga kuwa chaneli bora zaidi ya burudani kwa Watanzania na itaonyesha vipindi vipya mbalimbali vya burudani kama vile Bongo Movies, Bongo Swahili Series, Bongo Star Search, Bongo Secular Music (muziki wa bongo), Bongo Taarab, Bongo Comedies, Bongo Weekly Gossip, Bongo Gospel, Bongo Cooking Shows pamoja na vipindi vingine vingi. Chaneli ya Zuku Swahili Movies itabadilishwa kuwa Zuku Swahili namba 210, chaneli yenye vipindi mbalimbali za burudani kuanzia Novemba 13, 2016
Akizungumza katika uzinduzi, Meneja Mkuu wa Zuku TV Tanzania Bw. Omari Zuberi alisema, "Tunafurahia kuzindua kwa watanzania na wateja wetu muonekano mpya wa chaneli ya Zuku Swahili ambayo itatoa burudani bora zaidi za kibongo. Chaneli hii ni ushahidi wa dhamira yetu kwa watanzania na tumejipanga kukidhi mahitaji ya watazamaji na kujenga maudhui kwa wakati na kuvutia" alisema.
Chaneli ya Zuku Swahili inapatikana kwenye vifurushi vyote vya Zuku kuanzia kifurushi cha Zuku Smart kwa Tsh. 8,999, kifurushi chetu cha bei nafuu zaidi chenye chaneli zaidi ya 36 za bure ikiwa na chaneli za kitanzania na kimataifa na kupatia kipaumbele chaneli na mahudhui ya asili ya kiafrika.
Pia, Zuku TV itazindua filamu tatu mpya kupitia chaneli ya Zuku Swahili namba 210, filamu hizo ni Task Force Unit - (filamu ya upelelezi), Najifunga - (filamu ya hatma ya Albino) - na Wakoloni Weusi - (filamu ya rushwa katika Ofisi Kubwa ) na zinatarajiwa kuoneshwa mwezi wa Desemba 2016. Zuku imewekeza kwa asilimia kubwa na kuchangia ukuwaji wa sekta ya burudani na uzalishaji wa maudhui ya ndani Afrika Mashariki.
Kwa Tanzania, Zuku imewekeza zaidi ya TZS 21bn katika upatikanaji filamu za ndani ya nchi ambazo zimeonyeshwa katika nchi za Tanzania, Kenya, Zambia,Uganda na Malawi.
Wasanii nguli wa Filamu nchini Tanzania wakiongozwa na Chick Mchoma na JB walihudhuria uzinduzi huo. Chaneli ya Zuku Swahili itakuwa ni kituo chako cha burudani kwa filamu zote za Bongo.
Kwa Tanzania, Zuku imewekeza zaidi ya TZS 21bn katika upatikanaji filamu za ndani ya nchi ambazo zimeonyeshwa katika nchi za Tanzania, Kenya, Zambia,Uganda na Malawi.
Wasanii nguli wa Filamu nchini Tanzania wakiongozwa na Chick Mchoma na JB walihudhuria uzinduzi huo. Chaneli ya Zuku Swahili itakuwa ni kituo chako cha burudani kwa filamu zote za Bongo.
Pichani ni Raisi wa TAFF ndg. Simon Mwakifamba akizungumza na wageni waliohudhuria uzinduzi wa chaneli ya Zuku Swahili jijini Dar Es Salaam.
Mkurugenzi wa Zuku Tanzania, Ndg. Omari Zuberi akiongea jambo na Meneja msaidizi Zuku Tanzania, Bi. Veneranda Raphael katika uzinduzi wa Chaneli ya Zuku Swahili.
0 Comments
on