Suala la password ni suala la msingi sana katika kuhakikisha account yako ya Facebook au Instagram inakuwa salama.Japo wengi wetu tumekuwa tukileta mzaha mzaha na kujikuta account zetu zikivamiwa na wezi wa mitandaoni (Hackers). Nitaekeza Baazi ambayo kufanywa sana.Na endapo utayaepuka haya basi account yako itakuwa salama pia na data zako hazitavuja.
1:PASSWORD FUPI. Miaka mingi ya nyuma iliopita ilizoeleka password yenye namba/tarakimu 6 ni chaguo sahihi.Lakini kwa sasa kutokana na maendeleo/mapinduzi ya kitekinolojia Password yenye tarakimu/namba sita si salama tena ni lahisi wezi kuijua na kuingilia data zako.Chaguo dogo kwa sasa ni tarakimu 8 ,Japo nakushauri buni password yenye tarakimu 12.
2:PASSWORD RAHISI Endapo utaweka password ndefu afu ni rahisi mfano password ya "123456789" au "abcdefghijk" bado unafanya makosa na kupelekea account yako kuwa rahisi kuibiwa/kuingiliwa kwa sababu wezi wa mitandaoni wana fikilia mbali zaidi.Pia wana kamusi zenye password maarufu duniani hivyo kuandika password yenye maneno marahisi Kama "Iloveyou" ni makosa badala yake buni password yenye neno gumu pia liandikwe kwa kuchanganya herufi kubwa na ndogo pamoja na namba mfano "Eddwin1994" au "Photopoints2013" Hii haitakuwa rahisi kuchakachuliwa.
3:PASSWORD MOJA MITANDAO YOTE Inawezekana umebuni password ngumu kiasi kwamba unaona ni bora uitumie katika mitandao yote ili iwe rahisi kuikumbuka na kuihifadhi kichwani lakini kumbuka jambo hili lina athari kwa sababu ikitokea account moja imevamiwa na hackers basi account zako zote zitakuwa mikononi mwao ,Hivyo unashauriwa kuwa na password tofauti tofauti kwa mitandao tofauti tofauti .
4:KUIANDIKA SEHEMU Wengi baada ya kuzingatia kukwepa kosa namba moja na namba mbili hujikuta wakifanya kosa namba 4."Kuandika Password sehemu" mfano katika Daftari,Dairy,Notebook au hata ktk simu zao.Hili jambo si salama kwani yaweza siku ndugu/rafiki asiye muaminifu akaiba naye akaiweka vibaya ikasambaa na account yako ikawa haina usalama.Hushauri kuiandika password sehemu za wazi .
5.USIBADILI PASSWORD MARA KWA MARA Kuna watu wanatabia ya kubadili password Mara kwa Mara mfano kila baada ya miezi mitatu au sita lazma abadili. Kufanya hivyo hupelekea kutokuwa makini na kubuni password rahisi au fupifupi na kujikuta wakifanya kosa namba 1&2 Ushauri badili password inapotokea ulazima mfano labda umehisi account yako iliingiliwa.
0 Comments
on