Matokeo ya uchaguzi mkuu uliofanyika nchini Gambia yaliwaacha wengi vinywa wazi baada ya kiongozi aliyehudumu kwa muda mrefu kung’olewa madarakani.
Rais wa Gambia Yahya Jammeh alishindwa na mpinzani Adama Barrow kwenye uchaguzi huo kwa asilimia chache ya kura.
Adama Barrow alishinda uchaguzi huo kwa asilimia 45.5 ya kura dhidi ya Yahya Jammeh aliyepata asilimia 36.7 ya kura.
Kufuatia matokeo hayo, hatimaye uongozi wa rais Jammeh umefikia kikomo baada ya kuongoza kwa zaidi ya miaka 22 nchini Gambia.
Rais Jammeh pia anaarifiwa kupokea vyema matokeo hayo na kukiri kushindwa na Adama Barrow, jambo ambalo limeleta tabasamu katika nyuso za wananchi wengi wa Gambia.

0 Comments
on