vinundu-katika-vitufe-vya-f-na-j


Hebu tazama vitufe vya F na J katika keyboard yako.
Unaona nini?
Huenda sasa umeona toauti kati ya vitufe hivi na vitufe vingine vyote katika baobonye ya laptop au desktop yako.
Vitufe vya F na J vina alama maalum zinazoonekana kama vinundu.
1-sababu-za-vitufe-vya-f-na-j-kuwa-tofauti
Labda umewahi kuviona lakini kwa kuwa hukujua maana yake basi ukavipotezea tu. Lakini sababu ya kuwapo vinundu hivi zinaweza kukushangaza.
Endelea kusoma makala hii kufahamu sababu na kazi ya vinundu hivi katika baobonye ya kompyuta yako.

Sababu na umuhimu wa kuwapo kwa vinundu katika vitufe vya F na J katika Keyboard ya kompyuta

Baobonye zote zinazotengenezwa katika miaka ya karibuni zina herufi mbili zenye mwonekano wa kipekee.
Herufi za F na J zina nundu zinazoonekana kama vimsitari. Utaalam huu uliwekwa na mtu aitwaye E Botich. Vitufe hivi ni mwanzo wa mkusanyiko wa vitufe vinavyofahamika kwa kimombo kama home row keys.
Home row keys ni vitufe katika keyboard yako ambako vidole vyako hupaswa kukaa wakati unapokuwa hauandiki. Katika baobonye ya kawaida, vitufe hivi vimegawanyika katika pande mbili:
  • Kushoto ambako kuna vitufe vya A, S, D, na F
  • Kulia ambako kuna vitufe vya J, K, L, na ;
2-sababu-za-vitufe-vya-f-na-j-kuwa-tofauti
Unapoandika katika kompyuta, vidole vyako vinatakiwa kukaa kama inavyoonekana katika picha hii:
3-sababu-za-vitufe-vya-f-na-j-kuwa-tofauti
Hii ina maana kwamba vidole gumba vya mikono yote miwili vinatakiwa kugusa kitufe cha kuweka nafasi (space bar) ilihali vidole vya kwanza vinatakiwa kugusa herufi F na J.

Uwepo wa vinundu katika vitufe F na J ndipo unapohitajika …

Vinundu katika vitufe vya F na J vinakusaidia kuandika kwa urahisi zaidi. Ni kama vile vinahakikisha vidole vyako vinakaa mahali pamoja bila kutoka katika keyboard.
Vinakuwa kama mwongozo wa kuhakikisha vidole vya mikono yako vinakaa sawasawa bila kuhitajika kutazama baobonye unapokuwa unaandika.
Kwa ujumla kazi ya vitufe vya F na J ni kuhakikisha kuwa unaandika kwa haraka zaidi bila  ya kutazama au kuhamisha mikono yako.
Kwa kuwa sasa unajua kwa nini vinundu vimewekwa katika keyboard yako, weka basi hakikisha unavitumia kukusaidia kuandika kwa haraka na kwa urahisi zaidi.