mkutano wa hadhara kwa Mbunge wa Iringa Mjini,
Mchungaji Peter Msigwa, lakini limeweka
mlolongo wa masharti ambayo atalazimika kuyatii
kuepuka rabsha.
Wakati Jeshi la Polisi likitoa masharti hayo,
Mwanasheria Mkuu wa Chadema, Tundu Lissu
amesema vyama vya upinzani vitaendelea
kuendesha mikutano ya hadhara licha ya kufungua
kesi Mahakama Kuu ya kupinga zuio la shughuli
hizo, huku akisema amri ya kuzuia wanasiasa
kufanya mikutano nje ya maeneo yao imetolewa
bila ya kusoma sheria.
Mkoani Iringa, Jeshi la Polisi lilitoa masharti hayo
baada ya Msigwa, ambaye anaongoza Jimbo la
Iringa Mjini kwa kipindi cha pili mfululizo, kutaarifu
kuwa atafanya mkutano wa hadhara kuanzia
Septemba Mosi, siku ambayo Chadema imepanga
kuanza operesheni ya nchi nzima inayoiita “ya
kupinga udiktekta Tanzania”.
Katika barua aliyomwandikia Mchungaji Msigwa
juzi, Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Iringa (OCD), Y.
Z Mjengi amerejea barua ya mbunge huyo yenye
kumbukumbu namba MB/IR/M/05 ya Agosti Mosi
mwaka huu, inayohusu mikutano ya hadhara
kuanzia Agosti 3 hadi 22, ikianza saa 8:00 mchana
hadi 12:00 jioni.
Kupitia barua hiyo, ambayo Msigwa alithibitisha
kuipokea, Jeshi la Polisi limesema limeridhia kwa
sababu lengo la mkutano wake ni kuhamasisha
maendeleo na kupokea kero za wananchi, kazi
ambayo inatakiwa kufanywa na mbunge wa eneo
husika.
“Natarajia mkutano wako (Msigwa) utakuwa wa
amani na utulivu bila kumkashifu mtu wa chama
kingine,” anasema Mjengi katika barua hiyo.
“Mikutano yote hiyo kibali kimetolewa kwako kama
mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini. Sitarajii mtu
mwingine kutoka nje ya Mkoa wa Iringa kuja
kukusemea kuhusu maendeleo ya jimbo lako au
kuja kupokea kero za wananchi wako na kuzijibia
wakati hiyo ni kazi ya mwenye himaya ambaye ni
wewe.
“Kashfa, kejeli, matusi na maneno ya uchochezi
kwa viongozi wa Serikali vitahesabiwa ni uvunjifu
wa amani na hatua kali za kisheria zitachukuliwa
dhidi yako na zitapelekea kuzuiliwa kufanya
mikutano yako inayoendelea.”
Barua hiyo inaishia kwa maneno yaliyoandikwa
kwa herufi kubwa. “Kumbuka: Amani ya Tanzania
italindwa na kila Mtanzania kwa hiyo ni jukumu lako
wewe Mhe. Mbunge kutekeleza jukumu la ulinzi wa
amani. Kwa pamoja tutaweza,” inasema barua
hiyo.
Alipoulizwa kuhusu masharti hayo, Mchungaji
Msigwa alisema hayo ni ya kwanza lakini hakutaka
kuzungumza zaidi kwa maelezo kuwa alikuwa
kwenye kikao.
Msimamo wa Lissu
Hata hiyo, Lissu alisema muda mfupi baada ya
kesi yake kuahirishwa jijini Dar es Salaam kuwa
suala hilo halikubaliki kwa kuwa sheria
inawaruhusu kufanya mikutano popote.
“Mbona huniulizi kama Magufuli yuko sahihi
anaposema kila mmoja akafanye mikutano kwenye
kajimbo kake?” Lissu aliwauliza waandishi nje ya
Mahakama ya Kisutu akionekana kutaka
kuzungumzia suala hilo baada ya kuulizwa swali
tofauti.
“Sheria ya Tanzan ia inasema chama kilichopata
usajili wa kudumu kina haki ya kufanya mikutano ya
hadhara mahali popote,” alisema.
Alisema chama chenye usajili kina haki kufanya
mikutano na kwamba Rais Magufuli alitangaza
zuio hilo bila ya kusoma sheria.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa
mujibu wa Katiba ya nchi hii na sheria zake zote,
hana mamlaka yoyote ya kusema lolote au kufanya
lolote kuhusiana na mikutano ya hadhara,”
alisema.
“Mtu anayetambuliwa na sheria kuhusiana na
mikutano ni OCD peke yake.”
Lissu alisema kuweka mipaka hiyo kwa wanasiasa
kufanya shughuli zao kwenye maeneo waliyoshinda
tu, itawanyima haki viongozi ambao vyama vyao
havikupata ushindi, akitoa mfano wa Augustine
Mrema, ambaye ni mwenyekiti wa TLP na John
Cheyo (mwenyekiti UDP), kufanya shughuli za
siasa.
Lissu pia alizungumzia uamuzi wao wa kutangaza
mikutano ya hadhara nchi nzima wakati wakiwa
wamefungua kesi kutaka tafsiri ya Sheria ya Vyama
vya Siasa.
“Kesi mahakamani, maisha hayasimami. Hatuachi
kuwa chama cha siasa, hatuachi kuwa na haki zetu
kama vyama vya siasa. Haki zetu zinabaki
palepale,” alisema Lissu alipoulizwa sababu za
Chadema kutangaza mikutano ya hadhara kabla ya
uamuzi wa kesi yao haujatoka.
“Na kwa mujibu wa sheria, na sheria yenyewe ni ya
Vyama vya Siasa, ni kwamba vyama vya siasa vina
haki ya kufanya maandamano na mikutano ya
hadhara kwa mujibu wa sheria.
“Kwa hiyo tutafanya maandamano na mikutano nchi
nzima, si kwa sababu tumefungua kesi tu, bali kwa
sababu tuna haki kwa mujibnui wa sheria za
Tanzania kufanya maandamano na mikutano, kama
alivyo na haki mwenyekiti mpya wa CCM bwana
Magufuli, kama alivyo na haki bwana ole Sendeka
(msemaji wa CCM), kama alivyo na haki kiongozi
wa chama chochote kilichosajiliwa.”
Alisema hawawezi kuacha kutumia haki yao
ambayo ipo kisheria kwa sababu tu Mahakama
haijatoa uamuzi.
Kesi ya uchochezi
Jana, katika kesi nayomkabili Lissu, upande wa
mashtaka umeieleza Mahakama ya Hakimu Mkazi
Kisutu kuwa mshtakiwa huyo alikiri mbele ya polisi
kutenda kosa la kutoa maneno ya uchochezi.
Wakili wa Serikali, Bernard Kongola alisema hayo
wakati akimsomea Lissu maelezo ya awali ya kesi
ya kutoa maneno ya uchochezi.
Hata hivyo, Lissu aliyakana maelezo hayo na
badala yake katika maelezo hayo alikubali
utambulisho wake tu, yaani jina lake na wadhifa
wake kuwa ni mbunge.
Baada ya kusomewa maelezo hayo na kukana
mashtaka hayo, Hakimu Dk Yohana Yongolo
anayesikiliza kesi hiyo aliiahirisha hadi Agosti 24
wakati upande wa mashtaka utakapoanza kutoa
ushahidi.
Akimsomea maelezo ya awali, Wakili wa Serikali
aliieleza mahakama kuwa Lissu alitenda kosa la
kumuita Rais Magufuli kuwa ni dikteta Juni 28,
2016 katika eneo la mahakama hiyo, alikokuwa
amekwenda kwenye kesi nyingine ya jinai.
Wakili Kongola alinukuu maneno hayo kuwa
alisema: “Mamlaka ya Serikali mbovu ya kidikteta
uchwara yanapaswa kupingwa na kila Mtanzania
kwa nguvu zote. Huyu dikteta uchwara lazima
apingwe kila sehemu kama uongozi utafanywa na
utawala wa kijinga, nchi itaingia kwenye giza
nene.”
Wakili Kongola alisema kuwa Juni 29, 2016,
mshtakiwa huyo alikamatakwa akiwa nyumbani
kwake Tegeta Kibaoni wilayani Kinondoni, Dar es
Salaam na kwamba alipohojiwa alikiri kutamka
maneno hayo.
Jana nje ya mahakama, Lissu aliwashukuru wafuasi
waliofurika kushuhudia kesi hiyo akisema ni ishara
nzuri na kwamba watamaliza kesi zote
zinazowakabili kwa kufurika kwa wingi
mahakamani na hivyo kuwa kero

0 Comments
on