Header Ads Widget

Tahadhari Kwa Wakenya : Uchawi Ni Utumwa.

Na. THEOFLIDA WA YESU.
Naanza kwa kuwasalimu kwa JINA LA YESU.
Jina lililo Kuu kupita majina yote.
Wiki kadhaa zilizo pita, niliandika waraka
wangu kwa watanzania na kuusambaza
kupitia blogs na mitandao mbalimbali kuhusu
athari za kujihusisha na masuala ya waganga
wa jadi .
Katika waraka huo niliwatahadharisha
watanzania kutojihusisha na WAGANGA WA
TUNGULI kwa sababu WAGANGA WA TUNGULI
ni WACHAWI NA MAWAKALA WA SHETANI
walio vaa kofia ya utabibu.
KUUSOMA WARAKA HUO, TAFADHALI
TEMBELEA
: http://shuhudazaajabu.blogspot.co.ke/2016/07/
ushuhuda-nilimlisha-mume-wa-mtu.html
AU
http://www.mpekuzihuru.com/2016/07/ushuhuda-
nilimlisha-mume-wa-mtu.html
Katika waraka huo niliwaelezea watanzania
jinsi nilivyo shawishika kutafuta msaada wa
maisha yangu kwa MGANGA WA TUNGULI
aitwae MUNGU WA KABILI na kujikuta
nikipata matatizo makubwa ambayo hata
hivyo yalipelekea kunikutanisha na YESU
ambae ameniokoa.
Katika waraka huo nili sahau kueleza mambo
makuu mawili yafuatayo:
Kwanza nilisahau kuweka mawasiliano ya
MUNGU WA KABILI ayatumiayo pindi
anapokuwa nchini KENYA ili kuwa tahadharisha
wakenya wasipige namba hiyo wala wasijaribu
kutafuta msaada kwenye namba hiyo, kwa
sababu mtu huyo ni WAKALA WA SHETANI
alie jificha kwenye kivuli cha UGANGA...
Wengi walio jaribu kutafuta msaada kwa
MUNGU WA KABILI wamejikuta wakiishia
kuunganishwa na UTAWALA WA KUZIMU
ambao umewapelekea kujikuta katika matatizo
makubwa kama niliyo yapata mimi.
Nimeona vyema kuwatahadharisha wakenya,
kwa sababu mungu wa kabili hufanya kazi
zake Tanzania na Kenya. Anapokuwa Tanzania,
namba yake huwa ni + 255 744 000 473 na
anapokuwa Kenya , namba yake huwa ni +
254 704 71 61 59 .
Hivyo basi Ndugu zangu Wakenya , hii ni
tahadhari yangu kwenu. Nimeweka namba hizo
hapo juu kama alama ya MPINGA KRISTO
ambayo watu wote wenye hofu ya Mungu
wanapaswa kuepukana nayo..
Nimeongozwa katika namna ya rohoni, kuanza
kufanya kampeni ya nguvu dhidi ya roho ya
kuhusudu masuala ya UGANGA, UCHAWI NA
USHIRIKINA na nitajikita zaidi katika
mapambano dhidi ya MGANGA WA JADI
AITWAE MUNGU WA KABILI.
Ninaanza kwa kupambana na MUNGU WA
KABILI kwa sababu, kwa miaka zaidi ya
mitatu ambayo nimekuwa nikishirikiana na
MUNGU WA KABILI, nimeweza kujua kuwa
yeye ndio MKUU WA WAGANGA NA
WACHAWI WOTE WA AFRIKA MASHARIKI NA
KATI , na watu wenye hekima wanasema
katikati ya kundi la kondoo MPIGE RUNGU
MCHUNGAJI, NA KONDOO WOTE
WATATAWANYIKA.
Naamini nikimsambaratisha mungu wa kabili,
basi itakuwa rahisi kwa waganga wengine kwa
sababu wote ni kama wafuasi wake tu.
Katika kampeni yangu hii ya kiroho,
nimeanzisha blogu iitwayo SHUHUDA ZA
AJABU ambayo inapatikana :
www.shuhudazaajabu.blogspot.com .
Nitakuwa nikitoa shuhuda za mambo
mbalimbali ya kichawi niliyo fundishwa na
MUNGU WA KABILI na jinsi unavyo weza
kujiepusha nayo kwa kutumia Jina la Yesu.
Najua kazi hii itainua uadui mkubwa dhidi
yangu, kwa sababu hakuna kitu wachawi
wanakichukia kama siri zao kutolewa hadharani,
lakini kwa Jina la Yesu, nitapambana vita hii
na nitaishinda.
MUNGU WA KABILI na jeshi lake watajaribu
kushindana na mimi lakini hawatashinda.(
YEREMIA 1:19 .)
Shuhuda nitakazo zitoa, zitakuwa na
mafundisho mazuri yatakayo kupa faida , kama
Mungu anavyo sema katika kitabu cha ISAYA
48 kwamba " MIMI NI MUNGU
NIKUFUNDISHAE ILI UPATE FAIDA'.
Ushuhuda huu utakufanya umjue shetani vizuri
kama wasemavyo watu wenye hekima " MJUE
ADUI YAKO KAMA UNAVYO IJUA NAFSI
YAKO"
JAMBO LA PILI na la msingi ambalo
sikuweza kulielezea kwa kina katika waraka
wangu wa kwanza ni namna ambavyo
MUNGU WA KABILI alinifundisha uchawi na
uganga...
Nianze kwa kurudisha kumbukumbu zenu
nyuma. Kama mlifatilia vizuri waraka wangu
mtakuwa mnakumbuka kuwa, kwa kutumia
uchawi nilio pewa na MUNGU WA KABILI,
nilifanikiwa kuteka na kudhulumu mali za
mwanaume mume wa mtu aitwate " K".
Mali hizo zilikuwa ni pamoja na maduka
mbalimbali ya biashara ambayo nilimkabidhi
mdogo wangu ayasimamie.
Kutokana na usimamizi wa hovyo ulio fanywa
na mdogo wangu, maduka hayo yakaanza
kufilisika taratibu. Hali hii ilinifanye niende
kuomba msaada wa MUNGU WA KABILI.
Mungu wa Kabili akaniambia kuwa mimi
siwezi kufanikiwa kupitia biahsra yoyote hata
iweje. Mungu wa Kabili akaniambia , Nina
nyota ya Uganga " kwa hiyo ninatakiwa kuwa
mganga.
Sikuwa na jinsi zaidi ya kukubaliana nae kwa
sababu nilishamfanya kuwa kama muungu wa
maisha yangu. Nilitii na kufuata kila alicho
kisema.
Ikapangwa siku rasmi ya mimi kusimikwa
uganga kisha baada ya kusimikwa uganga
ndipo nianze kufanya kazi ya kuwaagua watu
wenye shida, tabu na matatizo mbalimbali ya
kimaisha.
Zoezi la kunisimika uganga rasmi lilikamilika
ambapo nilikabidhiwa nyenzo za uganga
pamoja na jina la kazi, baada ya hapo,
mungu wa kabili akaniambia, nitaanza
kufundishwa uganga, lakini akasema, kabla ya
kuujua uganga ninatakiwa kuujua kwanza
uchawi, kwa nadharia na vitendo. Hapo ndipo
ninaposema siku zote kuwa MCHAWI NA
MGANGA LAO MOJA.
mungu wa kabili aliniambia ' UCHAWI NI
SAYANSI YA SIRI YENYE MRENGO WA
UFISADI ( YANI MLENGO WA UHARIBIFUI )
Ilihali UGANGA NI SAYANSI YA SIRI YENYE
UWEZO WA KUPAMBANA ATHARI ZA NGUVU
YA SAYANSI YENYE MLENGO WA UFISADI.
mungu wa kabili akaniambia, ili niwe na
uwezo wa kupambana na uchawi ni lazima
kwanza niufahamu uchawi vizuri kwa nadharia
na vitendo , kisha baada ya hapo
nitafundishwa kuhusu mbinu za kupambana na
uchawi ambao kwa mujibu wa mungu wa
kabili, ndio huo uganga wenyewe..
Nilifundishwa vitu sana katika uchawi, kuanzia
jinsi ya kuroga ukoo mzima, kufanya watoto
wasikue, kutengeneza ukimwi wa kichawi,
kuvunja ndoa, kutengeneza radi, nyoka, simba
n.k, kusafiri na aina tatu za ungo wa kichawi,
kutengeneza na kuzuia mvua, kuchukua
misukule, kutengeneza magonjwa mbalimbali
kwa watu, mimea na mifugo, kutengeneza
chuma ulete, kutengeneza majini,kuingia
mikataba na majini & mizimu, kuwafunga watu
vifungo vya kichawi vya aina mbalimbali
nakadhalika....
==> NITAENDELEA KUSIMULIA KESHO.
Nitakuwa nikisimulia kila siku kupitia blogu
ya hapa MPEKUZI pamoja na blogu yangu
iitwayo WWW.SHUHUDAZAAJABU.BLOGSPOT.
COM .
MUNGU AKUBARIKI SANA..AMEN

Post a Comment

0 Comments