August 3 2016 Umoja wa vijana chama cha ACT-
Wazalendo umekutana na waandishi wa habari Dar
es salaam na kuzungumzia changamoto zilizopo
katika sekta ya elimu nchini ikiwa ni pamoja
kitendo kilichofanywa na serikali kwa
kuwasimamisha masomo wanafunzi wa Chuo kikuu
Dodoma (UDOM) wasiokuwa na sifa na baadae
kuwarudisha baadhi yao.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao
Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijana ACT-
Wazalendo amesema wanataka ufafanuzi wa
Serikali kuhusu ukweli kwamba ilifanya hivyo kwa
mashinikizo matatu ikiwa ni pamoja na kukosa
fedha za wafadhili.
Akizungumza kwa niaba ya wanachama hao
Kitentya Luth ambaye ni mratibu wa vijana ACT-
Wazalendo amesema…>>> ‘Katika uamuzi huo wa
kuwafukuza watoto wa kimaskini kutoka UDOM
kukaibuliwa lugha za udhalilishaji kwa kuwaita
Vilaza bila kuangalia athari za kisaikolojia ‘
‘ Sisi kwa nafasi yetu kama vijana tunalaani vikali
udhalilishaji huo mbali ya kulaani tunaitaka Serikali
ituambie na kutujibu masuala matatu yakiwemo ‘ –
Kitentya Luth
1. Je, ni kweli tatizo lilikuwa Udahili ambao
haukukidhi vigezo au ni ukosefu wa fedha
baada ya wafadhili kujitoa kama
tunavyosikia?
2. Mliwezaje kuwapata wanafunzi zaidi ya
300 mkidai wamekidhi vigezo vya kurudi
chuo na tunafahamu 7000 walikosa sifa
kwa matokeo yao kuwekwa hadharani?
3. Serikali imewapeleka wanafunzi katika
vyuo vingine, je, waliopelekwa walienda
kuendelea na elimu waliyoanza awali au
walikuwa na mwanzo mwingine