Hitmaker wa ‘Aje’ Alikiba amesema Kiki ni kitu ambacho hakipo kwenye menu yake.
Alikuwa akiongea kwenye kipindi cha Clouds 30 kupitia Clouds TV.
Kwanza kwangu mimi hicho kitu hakipo, sijui kusema mimi nina hela. Na
kuna watu wengine wanaongopa kwa kusema uongo tu kwasababu watanzania
tumeshakubali kupelekwa na hiyo,” alisema.
“Lakini kuna baadhi pia ya watanzania wapo makini sana, huwa hawakubali
kitu kirahisi na kuna wengine ni wepesi sana kuamini. Na hizi kiki
zinakuja kwasababu watu wanaamini. Mimi binafsi sitaki kabisa hivyo vitu
na sitokuja kufanya na kama kuna watu wanafanya hivyo vitu mimo
nimewaambia unajua kila mtu ana identity yake kwamba hawa ni watu wa
aina hii na hawa ni hii.”
Ukiongea kitu mtu mwenye akili zake timamu anajua kabisa hii si kweli na
Alikiba hawezi kufanya hivyo. Ila huyu anaweza kufanya hivyo na huyu
hawezi kufanya hivyo ila Alikiba anaweza fanya hivyo,” alisisitiza.
0 Comments
on