Mkali wa muziki wa RnB, Ben Pol amefunguka sababu inayoweza kuufanya wimbo ukawa mkubwa.
Muimbaji huyo amekiambia kipindi cha Planet Bongo cha East Africa Radio
kuwa wimbo ukiwa mzuri ni rahisi kuhit hata usipomshirikisha msanii
mkubwa.
“Kinachoboost wimbo si msanii bali ni wimbo wenyewe. Ukiangalia ‘Moyo
Mashine’ nimeimba mwenyewe umekuwa mkubwa, ‘Sofia’ niliimba mwenyewe
lakini wimbo ulikuwa mkubwa sana,” amesema Ben.
Ben Pol ameongeza kuwa kuwashirikisha wasanii wenye majina makubwa
hakufanyi wimbo ukapendwa zaidi ila ufundi uliotumika kwenye wimbo
wenyewe ndio utaufanya wimbo huo kupendwa. Kwa sasa wimbo wa ‘Moyo
Mashine’ umeendelea kufanya vizuri kwenye redio na TV japo una zaidi ya
miezi mitano tangu utoke...........................................................................
0 Comments
on