ILIPOISHIA
“Hembu Halima acha roho mbaya, tumekuja pamoja tutaondoka pamoja haiwezekani tumuache mwenzetu hapa”
Fetty
alizungumza kwa msisitizo na kuzidi kumchefua Halima. Bwana Rusev
akamuamrisha askari kuwasiliana na wezao walio ndani, naye akafanya
hivyo kupitia simu ya upepo. Taaa zote nje ya jumba hili zikawashwa, na
kuwafanya Fetty na wezake waonekane waliopo, Walinzi wapatao hamsini,
wakiwa na bunduki, waliiekekeza mitutu yao katika eneo walilo lala Fetty
na wezake na kuwafanya wanyanyuke taratibu huku mikono wakiwa
wameinyanyua juu.
ENDELEA
“Hichi ndicho mulichokua mukikihitaji?”
Halima
alizungumza kwa sauti ya kunong’oneza akionekana kukasirishwa na
kitendo hicho cha wezake kuwa wabisha hadi wametiwa nguviuni na
wanajeshi hjao wa bwana Rusev ambaye kwa mara ya kwanza walimuona ni mtu
mwema kutokana na ukarimu wake alio waonyesha kipindi akiwapoke na
kuzngumza nao hukusiana na biashara ya kuuza manohari waliyo fanikiwa
kuiteka kutoka katika jeshi la wana maji wa Tanzania.
Wakaamrishwa
kuelekea sehemu ambapo yupo Samson, akiendelea kulia kwa maumivu makali
aliyo yapata kutokana na risasi aliyo pigwa mguuni mwake.
Mr
Rusev akaagiza wapelekwe kwenye chumba chenye giza zito na wafungiwe
humo hadi kutakapo pambazuka ndipo ajue ni nini awafanye kwani siku zote
hua hapendelei mtu kugundua siri zake na isitoshe wao ndio walio
sababisha kwa makao makuu ya vikosi vyake kuweza kuvamiwa na jeshi la
nchi yake ya Russia na kusababisha vifo vya wanajeshi wake wengi sana.
Fetty
na wezake wakingizwa kwenye chumba chenye giza zito, hata kam ni jasiri
kiasi gini giza la chumba hicho ni lazima uogope kwani hata mtu wa
pembeni yako ha ta hauwezi kumuona zaidi ya kuisikia sauti yake.
***
Wakafika kwenye jumba la Frednando, ambalo lipo katikakti ya jiji la
Mexco, Raisi Praygod na Rahab wakapokelewa kwa heshimwa kubwa na
wafanyakazi wa Frednando ambao alisha wapa taarifa juu ya ugeni huo wa
rafiki yake kipenzi. Wakakaribishwa kwenye moja ya seble ambayo kuta
zake zimepabwa na madini ya dhahabu, huku sofa zake zikiwa
zimetengenezwa kwa mtindo ambao Raisi Praygod hakuwahi, kuuona katika
maisha yake
“Kaka uajua jumba lako ni zuri kuliko ikulu yangu?”
“Weee, acha utani kaka”
“Kweli vile Frednando, inanibidi nikirudi hivi Tanzania ikulu yangu niweze kuibadilisha, kidogo mfumo uwe kama huu wako”
“Ila unakumbuka kwamba ikulu si yako, ukimaliza kipindi chako anakuja mwengine?”
“Hata kama ila, kwa kipindi nitakacho kuwepo mimi itanibidi nikae kidogo sehemu ambayo ninaihitaji mimi”
Wakiwa
kwenye maongezi ya furaha, wahudumu wakawa na kazi ya kuandaa chakula
na vinywaji, kwa ajili ya wageni hawa. Kwa upende wa Rahab, kila kinacho
tokea kwake anaona kama ni ndoto, kwani hakutarajia ipo siku atakuja
kuishi maisha ya kuheshimiwa kama haya. Moyo wake ukajikuta ukiuchukia
ujambazi ambao alikuwa anaufanya na rafiki zake ambao hadi sasa hivi
ajui kama wapo hai, kwani kwa fununu alizo kua akizisikia, ni kwamba
marafiki zake hao nilazima waweze kunyongwa, hii ni kutokmna na uhalifu
mkubwa walio ufanya wa kuwaua askari wengi wa jeshi la polisi.
“Kuna klitu Frednando nahitaji kukifanya hivi karibuni?”
“Kitu gani?”
“Ninahitaji kumuoa Rahab wangu”
Rahab akastuka kusikia hivyo kwani hakutegemea kwamba inaweza kuwa jambo la haraka kama anavyo hitaji Raisi Praygod
“Waooo, kaka hilo ni jambo jema, tena unaonaje ukalifanya hapa hapa kwangu”
“Ndio
maana nikakuamnbia nahitaji kulifanya siku hizi za karibu, kutokana
nampenda sana Rahab, bila yeye nahisi kwa sasa ningekua marehemu”
“Kweli kaka, wewe sema ni lini unahitaji kumuoa, niweke mambo sawa si unajua tena”
“Huyu hana siku nyingi hata siku mbili hizi zijazo pia itakua ni sawa”
Rahab
akaachia tabasamu pana lililo zidi kuipendezesha sura yake iliyo
teumbwa vizuri kwa haraka haraka ukimtamza unaweza kusema ni binti wa
kirwanda aliye changanyia na msukuma, kwa maana, urefu amepewa, sura
ndio usiseme, hicho kiuno chake sasa, kimefungashia mzigo wa wastani wa
makalio yanayo mfanya awe na sifa zaidi ya sifa wanazo pewa asichana
wengine.
Raisi
Praygod na Rahab wakapewa chumba cha kupumzikia ambacho kina kila sifa
ya kuitwa chumba cha kuweza kulala Raisi Praygod pamoja na mkewe
mtarajiwa. Furaha ikazidi kutawala mioyoni mwao, kwani kila walipo kua
pamoja hawakusita kuipa miili yao burudani ambayo, Raisi Praygod,
alijikuta akizidi kuipenda kwani, mburudishaji alimjulia jinsi ya
kumburudisha.
***
Siku iliyo fwata, Fetty pamoja na wezake wakatolewa kwenye chumba
ambacho walifungiwa, hawakujua ni wapi alipo Samson, ambaye walimuacha
nje kipindi wakipelekwa kwenye chumba hicho. Wakafunga pingu mikononi
mwao pamoja na nyororo ndefu miguuni mwao. Wakapelekwa kwenye moja ya
chumba chenye kuta za vioo vigumu ambavyo si rahisi kuwez kumuona mtu wa
nje, ila mtu aliyopo nje unaweza kumuona.
Chumba
hicho hakikuwa na kitu cha aina yoyote, jambo lililo wapa alama ya
kuuliza kila mmoja kwamba humo ndani wameletwa kufanya nini. Mr Rusev
akaamrisha baunsa mmoja kuingia ndani ya chumba hicho kuweza kuwapa
mkong’oto mkali Fetty na wezake ambao wanaendele kushangaa shangaa.
Halima
akawa wa kwanza kuliona jitu refu si chini ya Futi nane likiingia ndani
ya chumba hicho, huku likiwa limejengeka kwa misuli mikubwa, huku
likiwa tumbo wazi na suruali ndefu, aaliyo ichimeka kwenye mabuti yake
makubwa ya kijeshi.
“Hei jamani chekini kule”
Halima
aliwaambia wezake ambao walikuwa wametazama pande nyingine ya chuma
hicho, kila mmoja akajikuta akitawaliwa na woga mwingi kiasi kwamba
wakaanza kurudi nyuma nyuma, huku wakilihofia jitu hilo linalo toa
mihemu mizito kana kwamba limetoka kukimbia safari ndefu.
“Jamani tuweni pamoja”
Fetty
alizungumza na kuwafanya wote wanne wajiweke sehemu moja huku wakiwa na
wanalitazama kwa umakini jitu hilo lililo anza kupiga hatua za taratibu
kuwafwata walipo.
Jitu
hilo likarusha ngumi ambayo, ilimpata Anna na kumuangusha chini huku
akitoa ukelele mkali, wa maumivu kwani ngumi hiyo ilimpata begani. Mr
Rusev na watu wake waliopo nje ya chumba hicho wakashangilia kwa kitengo
cha jitu hilo walilo lipachika jina la Great Lundark.
“Anna nyanyuka”
Halima alizungumza huku akimpa mikono yake miwili, Anna na kumnyanyua kutoka katika sehemu ambayo ameanguka.
“Jamani tuweni makini, tutawanyike”
Fetty
alitoa agazo ambalo kila mmoja alilitekeleza na kumzunguka jitu hilo,
kutokana na minyororo mirefu waliyo fungwa miguuni iliwasaidia kuweza
kupiga ndefu kiasi, Fetty akajirusha juu na kwakurumia pingu yake,
akaipitisha kwa haraka kwenye kichwa cha jitu hilo, na kuanza
kuning’inia kwa kwa mgongoni, na kulifanya jitu hilo kuanza kutapatapa,
huku likijaribu kuiweka mikono yake shingoni, ili pingu hiyo isiendelee
kumuumiza kuromeo lake. Halima na Agnes wakawa na kazi la kupiga magoti
ya jitu hilo na kulifanya lianza kuyumba.
Anna
kwa hasira akalisogelea na kwakutumia mikono yake akalibamiza kwenye
sehemu zake za siri na kulifanya litoe ukelele mkali. Anna akarudia tena
kulibamiza kwenye sehemu za siri na kuzidi kulifanya jitu hilo kuyumba
yumba. Fetty akazidi kutumia nguvu zake kuendelea kuivuta kwa nyuma
shingo ya jitu hilo, huku miguu yake akiwa ameikunja na kukanyaga kwenye
makalio ya jitu hilo, lililo anza kuishiwa nguvu.
Kwa
usirikiano wao wakaweza uliangusha chini jitu hilo, hapo ndipo ikawa
nafasi nzuri kwa Fetty kuimalizia kuivunja shingo ya jitu hilo na
kuwashangaza bwana Rusev na watu wake waote ambao hawakutegemea kwamba
jitu lao linaweza kufa.
Bwana
Rusev akaagiza wapelekewe majitu mengine mawili yanayo fanana na jitu
hilo walilo liua. Majitu mengine ambayo kwa jinsi yalivyo unaweza kuyapa
jina la magoliati, hii ni kutokana na urefu wao na miili mikubwa waliyo
nayo. Ikaingia ndani ya chumba huku ikiwa imeshika silaha mikononi
mwao, huku wakionekana kuwa na hasira kali ya mwenzao kuuawa.
SHE IS MY WIFE(34)
Ikwa
ni kazi kubwa sana ya Fetty na wezake kujiweka sawia kuhakikisha
wanapambana na mijitu hiyo ambayo kusema kweli, ikikubahatisha
kukutandika konde moja litakupa maumivu makali sana ambayo kuyavumilia
kwake ni lazima machozi yakulenge lenge.
Fetty
na Anna wakajiunga kupigana na jitu moja, huku Halima na Agnes
wakaungana kupambana na jitu la pili. Haikuwa kazi rahisi kwako kuweza
kupambana na majitu hayo yenye yenye silaha mikononi. Kwa bahati mbaya
Fetty akatandikwa ngumi moja kifua iliyo muangusha chini na kujkikuta
damu zikimtoka mdomoni.
Anna
kuona hivyo akarusha teke kali lililo piga sehemu za siri za jitu hilo
na kulifanya litoe mguno wa maumivu huku likijikunya na kumpa nafasi
nzuri Anna kuweza kuufikia uso wake. Kwa kutumia vidole viwili vya mkono
wa kulia, Anna akavisokomeza kwa nguvu kwenye jicho la kushoto la jitu,
akavitoa kwa nguvu na kuchomoka na jicho lote jambo lililo wastua bwana
Rusev na wanajeshi wake
“Arrhgaagaa”
Jitu
hilo lilitoa mlio wa maumivu huku, likiitupa silaha yake chini, na
kupiga goti moja chini, huku likiendelea kulia kwa maumivu makali
Anna
akaokota panga kubwa la jitu hilo na kulishika kwa mikono miwili, hii
ni kutokana na uzito wake, akamtazama jitu hilo linalo endelea kuvujwa
na damu nyingi kwenye jicho lake alilo lichomoa dakika mbili zilizo
katiza.
“Mother Fu….”
Jitu
hilo lilimtusi Anna na kumpa hasira kali ya kulipitisha panga hilo
kwenye shingo yake na kulitenganisha jitu hilo kichwa na kiwiliwili,
jambo lililo zidi kumuogopesha bwana Rusev na watu wake na kujiuliza
hawa wasichana ni watu wa aina gani.
Jitu
linalo pambana na Agnes na Halima, likazidi kuwaadamisha mabinti hawa,
kila mmoja amemshika shongoni mwake na mkunyanyua juu na kuendelea
kuwababiza ukutani mwa chumba hichi kilicho tengenezwa kwa vioo vigumu
sana.
Kila
walipo jitahidi kujitoa mikononi mwa jitu hili walishindwa, na kila
wanapo bamizwa ndivyo nguvu za mwili zinavyo waishia na kujikuta
wakitokwa na damu za pua.
“Ha..lima na Ag..nes wana…kufa kule”
Fetty
alizungumza kwa sauti ya kukata kata huku akinyanyua mkono wake wa
kulia akimuonyesha Anna kwa kutumia kidole sehemu wanapo sulubiwa wezao
hao wawili ambao wapo kwenye hatari ya kupoteza maisha.
Anna
kwa haraka akaanza kutembea huku mkono wake mmoja ukiliburuza panga
hilo refu kuelekea walipo wezake, kitendo cha Anna kulikaribia jitu
hilo, akaushirikisha mkono wake wa pili kulikamata panga hilo, na
kwakutumia nguvu zake zote akalipeleka kwenye mguu wa kushoto wa jitu
hilo, akautenganisha na mwili wa jitu hilo na kumfanya awaachie Halima
na Agnes, na wakaanguka chini. Kwa hasira kali Anna akaanza kulikata
kata jitu hilo kwa panga hilo kali, akazidi kulilarua huku akipiga
makelele ya uchungu, kiasi kwamba akazidi kulitesa jitu hilo, linalo
endelea kupiga makelele ya kuomba msaada wa walipo nje
“Ahaaaaaagrahhh”
Anna
alipiga ukelele huku akilishusha kwa nguvu zake zote panga kwenye
shingo ya jitu hilo na kulitenganisha kabisa kichwa mwili wake. Anna
akalitupa panga hilo chini na kujikongoja hadi walipo Halima na Agnes,
ambao kila mmoja anahema juu juu, kiasi cha kuwa katika hali mbaya sana.
Fetty taratibu akajinyanyua na kwenda walipo wezake na kukumbatiana kwa
pamoja huku machozi yakiwamwagika kwa uchungu mwingi, kwani wanapitia
katika kipindi kigumu cha maisha.
”Bosi tuwapige risasi wafe?”
Mlinzi
wa bwana Rusev aliuliza kwa lugha ya kirusi, bwana Rusev hakutoa jibu
lolote zaidi ya kuendelea kuwafikiria wasichana hawa jinsi walivyo
majasiri katika kupambana.
“Mkuu tuwaue tu hawa”
Askari
mwengine alizungumza kwa hasira huku akionekana akiikoki bunduki yake.
Kwa haraka bwana Rusev akachomo bastola yake na kumtandika risasi ya
kichwa askari huyo, aliye koki bunduki yake kwa ajili ya kutaka kwenda
kuwaua Fetty na wezake. Askari wote wakashangaa, na kujikuta wakimtazama
mwenzao huyo aliye lala chini huku damu zikumvuja kichwani
“Kuna mwengine anaye taka kwenda kuwaua hao mabinti”
Bwana
Rusev alizungumza kwa sauti ya ukali kwa lugha ya kurusi na kuwafanya
askari wake wote kukaa kimya, huku wakimtazama bosi wao huyo aliye
badilika na kuvimba. Bwana Rusev akapiga hatua hadi kwenye kitasa cha
mlango wa kuingilia ndani ya chumba hicho. Akakishika kwa nguvu na
kuufungua mlango huo na kuingia ndani huku bastola yake ikiwa mkononi,
akawafanya Fetty na wezake kustuka, na kujikuta wakimtazama bwana Rusev,
wakisubiri kupata hukumu yao kwa kuwaua majitu hayo
***
Siku ya harusi ya Raisi Praygod na Rahab, ikawadia huku ikiwa
imeudhuriwa na wasio zidi ishirini. Rahab katika siku alizo weza
kujikubali kuwa yeye ni mzuri, ni hii siku aliyo weza kuvishwa shele
lenye dhamani kubwa sana ya pesa. Aliweza kupambwa na mwanamitindo
waliye mpa kazi hiyo kutokea nchini Italia. Huku Raisi Praygod, akiwa
ndani ya suti nzuri iliyo tengenezwa na kiwanda maarufu nchini Italia,
na suti hiyo ina sifa za kipekee, ambayo mara nyingi huwa anaivaa raisi
wa Marekani.
Kwana
suti hiyo ina mionzi ambayo inaweza kuzuia risasi, ya aina yoyote
kuweza kumfikia mvaaji wa suti hiyo, pili ni suti ambayo inaweza
kuhimili mazingira yote ya hali ya hewa, kukiwa na joto sana inaweza
kukuba ubaridi kwenye mwili, kukiwa na baridi sana kunaweza kukupa ujoto
kwenye mwili wako.
Hawakuamua
kwenda kufunga sherehe hiyo kanisani bali walicho kifanya ni kumchukua
mchungaji ambaye akawafungisha harusi hapo hapo nyumbani, baada ya tukio
hilo muhimu la kufungishwa ndoa, wakafanya sherehe iliyo furahiwa na
kila mmoja, ni mpiga picha mmoja tu aliye kodishwa kwa kuifanya kazi
hiyo, huku watu wengine wakikataza kupiga picha hizo kutokana Raisi
Praygod hakuihitaji kuweka wazi uwepo wake kama yupo hai. Furaha kubwa
ikaendelea kutawala kwenye moyo wa Rahab ambaye hadi sasa hivi anajiona
mwanamke wa kipekee sana kwenye maisha yake kwa kumpata raisi Praygod
Frednando
akajitole kumzawadia rafiki yake huyo ndege aina ya Jet, aliyo inunua
siku chache kabla ya harusi kimya kimya, pasipo mtu yoyote kulifahamu
hilo. Ndege hiyo yakifahari ambazo zinamilikiwa na matajiti wachache
duniani, hua zinaingia abiria wasio zidi watano, huku kiwa inaendesha wa
marubani wawili, na nindege ambazo zinakwenda kwa kasi sana, na huwa
imekamilika kwenye idara kuanzia idara ya kujulinda kwa kuweza kufungwa
mitambo ambayo inazuia risasi na mabomu pale inapo kuwa imevamiwa
angani.
“Rafiki yangu, hii ndio zawadi yangu kwako na shemeji yangu”
Bwana
Frednando alizungumza wakiwa wamesimama kwenye kiwanja cha ndege
kilichopo kwenye kwenye eneo la jumba lake hili lakifahari. Wote watatu
wakaingia ndnai ya ndege hiyo huku wakiwa na furaha. Frednando
akawatambulisha raisi Praygod na Rahab kwa marubani wao ambao,
wameajiriwa kwa kazi ya kuiendesha ndege hiyo popote pale ambapo Praygod
na mke wake watahitaji kwenda.
“Tuzungusheni kidogo angani, ili wafaidi utamu wa ndege yao”
Bwana
Frednando alizungumza kwa lugha ya kimexco, marubani hao wakaifanya
kazi yao iliyo wafanya wawe hapo. Taratibu mashine za ndege zikaanza
kunguruma zikiashiria kwamba zinajiweka sawa kwa safari. Taratibu
ikaanza kutembea kwenye kiwanja hichi ambacho nikikubwa kiasi. Jinsi
ilivyo zidi kuongeza mwendo kasi ndivyo ilivyo anza kuiacha ardhi, huku
kila mtu akiwa amekaa kwenye kochi lake, lililo lililo tengenezwa
vizuri, huku pembeni kukiwa na kijimeza cha kuwekea juisi
“Unajua hii ndege, nimeinunua Dola milioni thelathini na tano”
“Duuu mbona pesa nyingi, hiyo inalisha nchi yangu”
“Ahaa
kawaida ndugu yangu kwa maana, kuna yakwangu kama hii nayo niliinunua
kwa bei kama hiyo seme zimetofautiana rangi, yangu ni nyeusi, nakumbuka
kuna siku uliniambia kwamba unapenda sana rangi ya silva, nikaamua
kukukamilishia moja ya ndoto zako”
“Asante sana Fred”
Wakiwa
juu angani, wakaendelea kupata vinywaji mbalimbali, huku wakitazama
baadhi ya chanel, za tv ndogo iliyopo kwenye kila meza ya safa lililopo
ndani ya ndege hiyo ya kifahari. Gafla Rahab akaanza kujihisi vaibaya
vibaya, huku mara kadhaa, akawa anajikaza ili Praygod asijue ni kitu
gani kinacho endelea, ila gafla akajikuta akianza kutapika na kulichafua
gauni lake alilo livaa
ITAENDELEA
0 Comments
on