Gazeti la Tanzania Daima limeripoti
kuwa Serikali imeanza uhakiki wa vyeti vya ndoa kwa watumishi wa umma.
Hatua hiyo ambayo imewashtua watumishi wengi wa umma, imeelezwa kuwa ni
mwendelezo wa harakati za Serikali ya Rais John Magufuli kuhakiki
watumishi wa umma ili kuondokana na watumishi hewa.
Wakati
Serikali ikianza na uhakiki wa vyeti vya ndoa, kazi ya uhakiki wa
watumishi hewa na vyeti vyao vya elimu inaendelea sehemu mbalimbali
nchini.
Kwa
muhibu wa Gazeti hilo, habari ambazo limezipata zinasema kuwa serikali
imeanzisha uhakiki huo nchi nzima kwa madai kuwa baadhi ya watumishi wa
umma wamekuwa wakitoa taarifa za uongo kwamba wana ndoa ili kupata nauli
na stahiki zingine za likizo wakati hawana ndoa.
Habari
zaidi zinasema kuwa walimu wakuu wa shule zote za Wilaya ya Ilala
wamepewa siku mbili kutekeleza agizo hilo kwa walimu wao.
Mmoja
wa walimu hao ambaye ameomba jina lake lihifadhiwe, alilithibitishia
Tanzania daima kuwa ametoa siku mbili kwa walimu wa shule yake wenye
vyeti vya ndoa waviwasilishe kwake.
"Kweli
tumepewa agizo hilo leo manispaa ya Ilala na tumetakiwa kuwasilisha
vyeti hivyo kesho na tayari baadhi ya walimu wangu wamefanya hivyo leo
na kesho zoezi hilo linakamilika"
Alipoulizwa
sababu ya kuwepo kwa zoezi hilo, mwalimu huyo alisema hajui lakini
anahisi lina lengo la kudhibiti taarifa za uongo za watumishi wakati wa
kuomba likizo.
Wakati
walimu wa shule za Ilala wakitakiwa kuwasilisha vyeti vyao vya ndoa,
wilaya nyingine za Temeke, Kinondoni, Ubungo na Kigamboni hawana taarifa
hizo.
Mmoja
wa walimu kutoka Manispaa ya Ilala alisema kuwa uhakiki huo una lengo
la kutaka kuchelewesha zaidi malipo na stahiki za walimu za likizo
ambazo hazijalipwa kwa miaka mingi.
0 Comments
on