Header Ads Widget

Viongozi waliopanga njama za kuwakeketa watoto wakike kukamatwa.

Serikali wilayani Tarime mkoani Mara,imeliagiza Jeshi la Polisi kanda Maalum ya Tarime na Rorya,kuwakamata na kuwachukulia hatua kali baadhi ya viongozi wa vijiji ambao wanadaiwa kushirikiana na wazee wa mila kupanga njama za kuwakeketa watoto wa kike wakati wa usiku.

Mkuu wa wilaya ya Tarime Bw Glorious Luoga,ametoa agizo hilo baada ya kuzindua bweni kwa ajili ya kuwahifadhi watoto zaidi ya 220 katika kituo cha Masanga ambao wamezikimbia familia zao kwa kuogopa kukeketwa,ambapo amesema kila kiongozi wa kijiji anapaswa kuwajibika katika eneo lake katika kudhibiti vitendo hivyo kutokea katika maeneo yao.

Naye Mkurugenzi wa kituo hicho cha Masanga kinachomilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Musoma Sista Stella Mgaya,amesema baada ya watoto hao kupokelewa katika kituo hicho,uongozi wa kituo utalazimika kuwatafuta  wazazi wao ili waweze kupewa elimu ya kuwawezesha kuachana na vitendo hivyo vya ukatili dhidi ya watoto wa kike.

Post a Comment

0 Comments