Kampuni hiyo imedai sababu hiyo imetokana na madhara ya nje ya simu ambayo yameripotiwa kusababisha simu kulipuka au kushika moto nchini China.
Imesisitiza kuwa simu hizo hazina tatizo lolote.
Kampuni inayofuatilia wateja ya Shanghai Ijumaa iliyopita ilidai kuwa imepokea ripoti nane hivi karibuni za iPhones kushika moto wakati zikitumika au zikiwa kwenye chaji.
Ripoti za kulipuka kwa simu hizo zimekuja miezi michache tu baada ya Samsung kupata hasara kubwa kutokana na kulipuka kwa simu za Galaxy Note 7 kiasi cha kusitisha kuzitengeneza.
Apple imesisitiza kuwa tatizo hilo haliwezi kuwa kubwa kama simu za Samsung.
0 Comments
on