Ukaribu wake kwenye mitandao ya kijamii siku za
karibuni unaweza kuwa ulikukutanisha na stori za
Diamond Platnumz kuwa amekua na uhusiano wa
kimapenzi na mwanamitindo wa bongo Hamisa
Mobetto.
Stori zilianzia kwenye birthday party ya mama
Diamond baada ya Hamisa kuonekana kuwa karibu
na familia hiyo hasa dada wa Diamond lakini pia
kuna picha iliyosambaa inaonyesha wawili hao kila
mmoja amepiga picha kwa wakati wake lakini
kwenye mazingira ya chumba yanayofanana
.
Diamond Platnumz ametolea ufafanuzi ishu hiyo na
kusema “Hamisa nimeanza kumjua zamani sana
kwasababu yupo katika industry hizi za kufanya
fashion, nimekua nikimjua muda mrefu kidogo na
sikuwahi kuwa na matatizo nae yoyote sababu
tumekuwa ni watu tu ambao tunaheshimiana ….. ”
"Sina uhusiano wa kimapenzi na yeye, juzi kati
alikua kwenye video yangu mpya nimefanya na Ray
Vanny na nafikiri hiyo imechangia kuingiza hayo
maneno, kufanya video Tanzania mara nyingi huwa
inaleta manenomaneno"
0 Comments
on