Mkuu wa wilaya ya Ilala, Sophia Mjema amezindua
kiwanja cha mpira wa kikapu na netball katika
shule ya sekondari ya wasichana ya Jangwani
kilichojengwa na mwanamitindo mjasiriamali,
Jokate Mwegelo.
Bi. Mjema aliwataka wanafunzi kutumia uwanja
huo kwa faida ya kukuza michezo pamoja na elimu
na kumpongeza Jokate kwa alichokifanya.
“Juu ya yote hayo uliyofanya lengo ni kutaka
watoto wa kike na wenyewe wawe na kiwanja cha
mpira hongera sana kidoti, hili jambo huwa sio
rahisi sana, tuna watu wangapi wanaweza
kutengeneza viwanja kama hivi hata kumi, lakini
wewe kwa kile kidogo ulichokipata ukasema hapana
mimi ujuzi wangu na experience na yale niliyopata
ngoja nisaidie,” , alisema Bi. Mjema.
Awali Mkurugenzi wa kampuni ya Kidoti, Jokate
Mwegelo alisema, “Mimi naamini michezo ni kitu
hamasishi kwa wanafunzi kufanya vyema pia katika
masomo yao na kufaulu ni wazi kuwa moja ya
changamoto kubwa nchini. Ukosefu wa viwanja
bora ambavyo hukwamisha wachezaji chipukizi
kuonyesha vipaji vyao ipasavyo,” alisema Jokate.
Alisema ataendelea kujenga viwanja katika shule
mbalimbali kwa faida ya wanafunzi. Jokate
ameshiriki ujenzi wa uwanja huo akishirikiana na
taasisi ya Modern Foundation.