MTUNZI: ENEA FAIDY
...... MR ALOYCE alibaki kimya akiwa ametulia
kimya kama vile amegandishwa na gundi ngumu.
Haja ndogo ilipita taratibu katikati ya mapaja yake
na kushuka chini ardhini.
Alitamani ardhi ipasuke ili walau akajifiche chini ya
ardhi kuliko kuendelea kushuhudia tukio lililokuwa
linaendelea kwa wakati ule.
Akili ilisimama, mwili ulinyong'onyea kwani
hakuwa na lolote la kuweza kufikikiria kwa wakati
ule. "Nimekamatika kwenye mtego" ndilo wazo
pekee lililomjia akilini mwake.
Chatu yule aliendelea kujiviringisha kwa madaha na
mbwembwe nyingi mwilini mwa Mr Aloyce na
kumfanya mwanaume yule ajihisi mfu aliyebakisha
roho yake tu kabla ya mazishi.
"Nisaidie Mungu wangu" Mr Aloyce alisali kimoyo
moyo akiamini kwamba huenda Mungu atasikia
maombi yake na kumkumkumbuka katika Mateso
yake. Machozi hayakumtoka hata chembe kwani
hofu ilimzidia mpaka chozi lilimkauka.
Akiwa katika hali hiyo ngumu isiyoelezeka Mr
Alloyce hakuona mtu yeyote wala dalili ya kiumbe
chochote katika eneo lile. Ghafla upepo mkali
ukapuliza eneo lile, ulikuwa kama kimbunga
kinachoweza kuleta maafa kwa makazi ya watu.
Mr Aloyce alijishangaa sana kuona mwili wake
ukiwa mwepesi sana tena umejiachia kupita kiasi.
Moyo wake ukafurahi na akatumia nafasi hiyo
kujitazama mwilini mwake, akagundua yule chatu
hayupo tena mwilini mwake Bali amesogea
pembeni kidogo na kujituliza kama gogo.
Macho yalimtoka kama njugu akimtazama yule
Chatu, ghafla akapigwa na mshangao wa ajabu
baada yule chatu kubadilika umbile na kuwa na
umbo la mtu. Mr Alloyce akamkazia macho MTU
yule aliyetokana na chatu.
Hakuamini macho yake pale alipogundua mtu yule
alikuwa mkewe, Aloyce alitetemeka sana. Ndipo
mwanamke yule alipoachia kicheko kikali sana
huku akimsogelea Mr Aloyce. "Nilikukumbuka sana
mume wangu.. Ila nasikitika unaniogopa" alisema
mwanamke yule mwenye sura na umbile la mama
Eddy. Mr Aloyce alitetemeka sana, akapiga hatua
za kinyumenyume kumkwepa mwanamke yule.
"Mume wangu! Mbona unaniogopa?" Alisema
mwanamke yule.
==>Endelea Nayo <<Kwa Kubofya
Hapa>>
0 Comments
on