Msanii
wa muziki wa kurap, Mr Blue amesema hahitaji kuwa na meneja wa
kumsaidia katika kazi zake za muziki kwa kuwa tayari alishawahi kuwa na
mameneja zaidi ya watatu ambao hawakumpatia mafanikio.
Rapa huyo ambaye anafanya vizuri na wimbo ‘Mboga Sana’ amesema alikuwa
hawezi kuishi kwenye tasnia ya muziki bila kuwa na meneja lakini
kutokana na kuona mchango wao kwake haukuzaa matunda.
“Mimi nilikuwa siwezi kuendesha maisha yangu ya muziki bila kuwa na
meneja na nilifanya kazi chini ya mameneja watatu lakini kwa sasa
nimesema basi sihitaji meneja tena nahitaji ushauri wa wadau namna ya
kuboresha kazi zangu,” Mr Blue alikiambia kipindi cha FNL cha EATV.
Rapa huyo pamoja na AliKiba wameshiriki kusapoti ngoma ya Abby Skills
inayokwenda kwa jina la Averina , ambapo Abby amewataka mashabiki
kumuunga mkono ili arejee vyema kwenye game kama zamani.
0 Comments
on