Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt.
John Magufuli wakati wa ziara yake mkoani Tabora
alitoa maagizo kadhaa kwa watendaji likiwemo
agizo la kufunguliwa kwa stendi ya mabasi Igunga
ambayo ilikamilika na kuacha kutumiwa kwa
miaka 10.
Kufuatia agizo hilo tayari SUMATRA kwa
kushirikiana na jeshi la polisi kikosi cha usalama
barabarani wameanza kuelekeza magari yote ya
abiria yanayopita Tabora eneo la stendi hiyo
kuhakikisha yanapita jambo ambalo limeanza
kufanyiwa kazi kwa vitendo.
Akizungumza wakati wa kukagua utekelezaji wa
agizo hilo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Aggrey
Mwanri amesema SUMATRA washirikiane na jeshi
la polisi kuhakikisha kila gari la abiria linapita na
dereva atakayekaidi agizo hilo anyang'anywe
leseni.
"Ni lazima mabasi yapite hapa stendi na yeyote
atakayekaidi SUMATRA chukueni hatua na jeshi la
polisi toeni ushirikiano kuhakikisha suala hili
linafanikiwa'' Amesema Mwanri.
Aidha kwa upande wao wananchi wamesema
watanufaika sana kufuatia stendi hiyo kuanza
kufanya kazi kwa kuwa watafanya biashara
mbalimbali kuzunguka stendi hiyo.
0 Comments
on