Header Ads Widget

Wafungwa Kifungo cha Maisha Jela Kwa Kumbaka Mama Mbele ya Mumewe na Watoto

MAHAKAMA ya Wilaya ya Mbarali mkoani Mbeya
imewahukumu kutumikia kifungo cha maisha jela
vijana wawili wakazi wa wilayani Chunya mkoani
humo kutokana na kosa la ubakaji wa mwanamke
mmoja waliyemtendea kitendo hicho mbele ya
watoto wake.
Kadhalika, mahakama hiyo imewahukumu vijana
hao wawili kutumikia kifungo cha miaka 30 jela
kutokana na kosa la unyang’anyi wa kutumia
silaha ambapo siku ya tukio walimjeruhi mume wa
mwanamke waliyembaka.
Vijana waliokumbwa na vifungo hivyo viwili
kutokana na mashitaka mawili yaliyokuwa
yakiwakabili ni Ngaru Joseph (32) na Pili Mneme
Kapigi (30) wote wakiwa ni wakazi wa wilayani
Chunya mkoani Mbeya.
Awali ilielezwa mahakamani hapo na Mwendesha
Mashitaka wa Jeshi la Polisi Mazoya Luchagula,
Mbele ya Hakimu Mfawidhi wa Mahakama hiyo
Alice Mkasela kuwa mnamo Julai 10, mwaka huu
saa nane usiku nyumbani kwa mlalamikaji katika
Kijiji cha Ukwavila wilayani Mbarali washitakiwa
walivamia na kuvunja mlango nyumba ya mkazi
huyo aliyekuwa amelala na mke na watoto wao.
Luchagula alisema walipofanikiwa kuingia ndani ya
nyumba hiyo washitakiwa hao walimjeruhi baba wa
familia kwa kumkata na shoka kichwani kisha
wakapora fedha kiasi cha Sh 580,000, wakachukua
nguo zote za wanafamilia na kisha kumbaka
mama wa familia mbele ya mumewe na watoto.
Mwendesha mashitaka huyo alisema wanafamilia
hao kupitia mwanga wa taa ya sola waliweza
kuwatambua watuhumiwa kabla wazazi
hawajapelekwa Hospitali ya Misheni Chimala
walikolazwa kwa ajili ya matibabu.
Kutokana na makosa hayo Luchagula aliiomba
Mahakama kutoa adhabu kali kwa washitakiwa ili
iwe fundisho kwa watu wengine walio na tabia
hizo wilayani hapa na kwingineko nchini.
Akito adhabu kwa washitakiwa, Hakimu Mkasela
alisema ameridhishwa na ushahidi uliotolewa
mahakamani hapo na pande zote mbili na kwamba
kwa kosa la kwanza la unyangaji wa kutumia
silaha washitakiwa watakapaswa kutumikia kifungo
cha miaka 30 jela na kwa kosa la pili la ubakaji
watatumikia kifungo cha maisha jela ili iwe
fundisho kwao na watu wengine.
Awali washitakiwa waliiomba Mahakama
kuwapunguzia adhabu wakisema bado umri wao ni
mdogo na wanategemewa na familia zao, maombi
ambayo yalitupiliwa mbali na hakimu Mkasela.

Post a Comment

0 Comments